Wednesday, December 6, 2017

Jinsi Ya Kuapproach Mwanamke Ambaye Humjui


Unataka kuzungumza na mwanamke ambaye humfahamu?
Kuongea na mwanamke ambaye humjui ni kama vile kujaribu kuoga na maji baridi.
Inakuwa vigumu na inakufanya kuingiwa na kibaridi. Kila wakati unapochukua hatua ya mbele unaskia kama tumbo linakukoroga vile.
Lakini kama mwanamume, jinsi ya kuapproach mwanamke ni jambo muhimu la kujua ikija maswala na kudate.
Kile ambacho kinachohitaji kwanza kabisa ni kumfanya mwanamke kama huyo akutambue...yaani upate attention kutoka kwake. Hii inakuwa rahisi kwa kutumia mbinu hizi:
1. Mwangalie
Tuseme sahizi uko na marafiki zako ama uko pekeako katika sehemu ambayo ina watu wengi halafu huyo mwanamke unataka kumuaproach yuko karibu na wewe ama sehemu mbali kidogo na wewe. Kile unachohitajika sasa ni umuangalie ili ufanye kumuonyesha kama unajaribu kumuangalia yeye. Jaribu kujifanya unamwuangalia kisirisiri, halafu akijaribu kukuangalia tu unajifanya unashughli nyingine ama unaongea na marafiki zako. Hii itamsisimua kutaka kujua kwa nini unamuangalia hivyo itamfanya na yeye kukuangalia mara kwa mara kama utakuwa ukimwangalia 
2. Mwangalie machoni
Kila wakati akikuangalia, wewe muangalie halafu papo hapo uangalie kando kikondoo. Endelea kumuangalia kimtindo huo mara kwa mara, na wakati mwingine, mwangalie nusu sekunde, uangalie kando halafu hapo hapo muangalie tena (nadhani hapo umenipata). Ukifanya hivyo utakuwa automatiacally unamsisimua kihisia. Lakini kama umejaribu njia hii yote halafu hakuonyesha dalili ya kuingiliana basi itakuwa hajakupenda ama kuridhika na wewe.
3. Jifanye kutoeleweka
Kama uko na marafiki zako, muangalie mara kwa mara, lakini jifanye kama unasumbuliwa na jambo fulani ambalo linakufanya wewe usielewe kile ambacho marafiki zako wanaongea. Hii itamfanya yule mwanamke kufikiria kuwa ameingia kwa akili yako hivyo ataona ya kuwa yeye ndiye chanzo kikuu kinachokuzuia wewe kumakinika na yale ambayo marafiki zako wanaongea. 
4. Mwonyeshe tabasamu
Bila kupoteza wakati, hii itakuwa ufunguo wa kwako kufungua mlango wako wa kuongea naye kwani atenshen yote yake itakuwa imekuja kwako hivyo lile unalohitajika la kufanya ni kumwonyesha tabasamu. Fanya kusmile kiasi tu ili kuonyesha kuwa wewe umekuwa intrested na yeye muda huyu wote.
ONYO: Usijaribu kuweka smile kubwa kwani itaweza kuleta maana nyingine haswa kwa mwanamke ambaye humfahamu kabisa.
Hatua hizi hapa juu lazima zote ziwiiane, yaani lazima zifanye kazi. Iwapo katika hatua yoyote hapo juu utamwona mwanamke anakupotezea, basi jua na mapema kuwa hujamridhisha na kile unachohitaji kufanya ni kukimbia tu.