Friday, December 22, 2017

Utafiti: Picha za Utupu Hupunguza Hamu ya Kufanya Mapenzi.


Watoto wengi hupata njia ya kutazama picha za ngono mitandaoni wakiwa na umri mdogo, kwa mujibu wa utafiti.

Karibu asilimia 53 ya watoto walio kati ya umri wa miaka 11 na 16 wametizama picha za ngono mitandaoni, wote wakiwa ni asilimia 94, ya walioona picha hizo wakiwa na umri wa miaka 14 kulingana na utafiti wa chuo cha Middlesex.

Utafiti huo unasema kuwa vijana kama hao, wako kwenye hatari ya kupoteza hamu ya kushiriki mapenzi.

Serikali inasema kuwa ili kuhakikisha kuwa watoto wako salama na masuala ya mitandao ni jukumu kubwa.

Watafiti waliwahoji watoto 1,001 walio na umri kati ya miaka 11 na 16, na kugundua kuwa asilimia 65 ya wale walio na umri wa kati ya miaka 15-16, walikubali kuona picha za ngono sawa na asilimia 28 ya wale walio kati ya miaka 11 na 12.