Monday, April 30, 2018
Epuka kufanya mambo hayo kwa mpenzin wako
Unapokuwa na mpenzi wako katika mahusiano, epuka sana kufanya vitu vya aina hii ambavyo vitasababisha mahusiano yenu kufa.
1. Kuanza kuchelewa kutoka kazini mara kwa mara.
Sio kwamba kila mtu anapochelewa kutoka kazini basi anakuwa sio mwaminifu, lakini zaidi ya asilimia 75 (kutoka kwenye tafiti) ya ambao wamekuwa na mahusiano nje wamekuwa wakitoa visingizio vinavyohusiana na kazi, vikao, mikutano na safari za kikazi, yamkini wewe ni shahidi wa hili.
2. Mazingira tatanishi ya simu :
Gafla simu zinaanza kumiminika mpaka mida ya usiku. Yamkini pia alikuwa yuko huru hata simu yake inapolia waweza ichukua na kumpatia lakini gafla anakuwa na hofu kubwa na kuificha simu yake, nimeongea na wengine ambao wanakwenda na simu hadi bafuni isije ikasikika.
Wengine wanaondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, kuwe siri (password) ngumu hadi mwenyewe anashindwa kuikumbuka, wako ambao simu zao zikipigwa hawawezi kupokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida, ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa.
3. Harufu ambazo hujazizoea
Kwa kuwa wapendanao huwa wamezoeana, maranyingi hata aina ya manukato mmoja anayotumia yanakuwa yanajulikana kwa mwenzake, Sasa hembu fikiri unamkuta mpenzi wako ametokea na ana harufu ya tofauti kabisa na uliyoizoea, umeisikia harufu hiyo akiwa amerudi toka kazini wakati asubuhi alipoondoka alikuwa na harufu ile uliyoizoea.
4.Tabia za kuanza kukufuatiliasana au hata kukuganda.
Wapo wanaotawapeleka wapenzi wao kila wanakotaka, nakutoruhusu mazingira ya wapenzi hawa wakike kuwa huru kufanya mambo yao wenyewe, wengine waliitafsiri hali hii kama penzi kubwa lakini baada ya muda unagundua kuwa ile ilikuwa ni ujanja wa kuficha uhalisi wake na kuzuia mazingira kwa mpenzi wake kugundua au kupewa taarifa ya tabia zake.
5. Kuzungumza sentensi za kutatanisha:
Unaweza kukuta katika mapenzi yenu mpenzi wako anaanza kuwa na sentensi ngumu na zisizo kuwa na msingi kwa mfano anasema “kwa jinsi hii sidhani kama tutafika” “mi siamini kama mapenzi yanadumu” “yani ndio maana watu wanashindwa kukaa na mpenzi mmoja” na maranyingine anaweza kukuuliza baadhi ya maswali moja kwa moja ili kukuona utajibuje. Sentensi hizi zina chanzo moyoni, kuwa macho.
6. Tabia za kuficha fedha:
Hii utaiona ghafla mpenzi wakeo anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwa ulizwa kuhusu suala hilo. Tabia hii ikidhihirika katika mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana kwa kukaa kimya unaweza kujikuta umechelea mwana na maji ya moto