Tuesday, December 5, 2017

HICHI NDIO KITU HATARI KATIKA MAPENZI NA FAMILIA


Anashindwa kujua kwamba fedha anazotafuta si zake peke yake. Kama anaona anatakiwa kutumia fedha zake peke yake, basi hapaswi kujipa mzigo wa kumiliki familia. Mtu anapokuwa baba au mama, uamuzi wake unatakiwa uwe kwa ajili ya wengi. Kumaliza mshahara kwenye kumbi za starehe ni ukatili kwa familia hususan mtoto ambaye hakukuomba umlete duniani. Usijidanganye kwamba unajimiliki mwenyewe. 
Wewe unamilikiwa na familia yako, kwa hiyo una deni na wajibu mkubwa kwa wale wanaohusika. Kabla ya kwenda nyumba ya kulala wageni na huyo unayemtamani, fikiria kwamba unamilikiwa. Baba au mama, anapokwenda hoteli na mpenzi wa nje. Akakubali kuvua nguo na 
kufanya mapenzi. 
Ajitambue kuwa anachezea maisha ya watu wengine. Kuna maradhi, kwa hiyo unatakiwa uwe na afya njema ili wanaokumiliki waendelee kupata huduma yako. Unafahamu kwamba mapenzi yanaua. Unaelewa kuwa unaposhindwa kuwa mtulivu nyumbani, unaiba muda wa familia yako. Kumbe sasa, fedha siyo zako ila ni za familia. Unaweza kupata picha kwamba viungo ni vyako lakini penzi si lako. Ukilitoa ni wizi, ni dhuluma