Tuesday, December 5, 2017

Utafiti: Wasichana wengi “watoa nyuma” kingono ili kutunza bikra, na kuepuka mimba


Utafiti juu ya ufanyaji wa ngono kinyume cha maumbile katika maambukizi ya UKIMWI, umeonyesha kuna idadi kubwa ya wasichana wanafanya tendo hilo. Baadhi ya wanawake waliohojiwa katika wilaya za Kinondoni, Tanga, Makete, na Siha, wamekiri kufanya tendo hilo linalojulikana mitaani kama tigo, huku wakidai sababu ni kuepuka mimba, au kutunza bikra. 
Utafiti huo uliofanywa na Mwanasayansi Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Mangojwa ya Binaadamu Tanzania (NIMR) ulihusisha wanawake wenye umri kuanzia miaka 15 na kuendelea, na asilimia 26, ambayo ni kama kila msichana mmoja kati ya wanne, walikiri kufanya tendo hilo. 
“Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume,” alisema Mtafiri Irine.
Katika wilaya zilizofanyiwa utafiti, wilaya ya Tanga ndiyo imekithiri kwa vitendo, na wilaya yta Makete ndiyo yenye idadi ndogo zaidi.
Wanaume waliohojiwa katika utafiti huo wamedai wao wanawafanyia wanawake vitendo hivyo kwa ajili ya kupata raha tu na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ikiwa ni hafifu kwani wakitumia mipira wamedai hupunguza raha wanayoipata.
Wanawake wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa za mwambao wa Tanga za msichana kuolewa na kukutwa na mimba au usichana wake (bikira) haupo, ni aibu kwake na wazazi hivyo huamua “kutoa nyuma” ili kuepuka kuiletea familia aibu kwa njia ya mimba, au kupoteza bikra.
Watafiti hao wameshauri elimu zaidi ya kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI na njia salama za kujamiiana kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya kujamiiana kinyume na maumbile kuwa haiambukizi VVU.