1# Kukosa siku zako za hedhi
Unaona mwezi mmoja ama zaidi umepita bila kuona siku zako za hedhi yawezekana utakuwa umenasa ujauzito,maana mtu mjamzito hawezi kupata hedhi mpaka atakapojifungua,kukosa hedhi pia husababishwa na sababu zingine kama kubadilisha mazingira,vyakula stress na mengine
2# Kichefuchefu na kutapika
Wakati mimba inapoanza kutunga kuna homoni ambazo huwa zinafanya kazi na huweza kusababisha kichefuchefu kwa mama mjamzito hali hii humfanya apate wakati mgumu kula baadhi ya vyakula,hii mara nyingi huanza wiki ya sita ya ujauzito japo hali hii si kwa kila mjamzito.
3# Kujisikia haja ndogo mara kwa mara
Muda si mrefu baada ya kushika ujauzito homoni hubadilika na huchochea msukumo wa damu na kupelekea mjamzito kujisikia kwenda haja ndogo za mara kwa mara
4# kubadilikabadilika kwa mood
Ni ile hali maarufu kwa wajawazito kubadilika hisia mara kwa mara saikolojia yao hubadilishwa na homoni za ujauzito na hujikuta wanakuwa na vituko vya kushangaza maana kuna wakati unaweza kuwa unacheka na mjamzito ila ghafla ananuna ama kulia au kukumbwa na hali ya uoga bila sababu yakueleweka,kama wewe ni mwanaume inabidi umvumilie tu mwanamke wako ,maana hali hii hutokea bila wao kupanga
5# Matiti kuvimba na kujaa
Wakati wa ujauzito matiti huweza kujaa hii huwa ni kwa ajili ya kuandaa chakula cha kiumbe kilicho tumboni kwa mama mjamzito hivyo chuchu huweza kusimama
6# kusumbuliwa na harufu mbalimbali
Hasa kama unapata mimba kwa mara ya kwanza utachukia harufu za vyakula na vinywaji au hata marashi ya aina fulani,wakati mwingine hata harufu za watu wa karibu na wewe
7# Kujaa mate mdomoni
Hii huchochewa na homoni za ujauzito hivyo mama mjamzito hujikuta anajawa na mate mdomoni yanayompelekea awe anathema mate mara kwa mara
8# Uchovu
Mara nyingi mwili wa mjamzito hupitia mabadiliko mbalimbali ambayo humfanya awe mchovu mara kwa mara na kujisikia vibaya kama mtu mwenye dalili za kuugua
9# Kusinzia ovyo
Uchovu anaoupata mjamzito humpelekea kupata usingizi wa mara kwa mara tofauti na hali yake ya kawaida kabla ya uzito ,anaweza kuwa na usingizi wa ghafla na mara kwa mara kama mtoto mchanga.
10# Kupata vitone vya damu sehemu za siri(spotting)
Kuna wakati unaweza kupata damu kidogo sana sehemu za siri kitaalamu hujulikana kama implantation bleeding,haijulikani hasa kwanini damu hii kidogo huwa inatoka wakati huu,ila mwanamke 1 kati ya 4 huweza kupata damu hii, wakati mwingine damu ya namna hiyo huweza kuwa dalili ya mimba iliyotunga nje ya tumbo la uzaziectopic preginancy
11# Joto la mwili hupanda kuliko kawaida
Kama ulikuwa unaweka kumbukumbu ya joto la mwili utaweza kuona joto la mwili wako linazidi kupanda kila siku kwa siku 18 na zaidi ,yawezakuwa umenasa umenasa.
12# Chuchu kubadilika na kuwa nyeusi
Chuchu zako zinaonekana tofauti kwa sasa? huwa inatokea mara nyingi wiki ya 10 ya ujauzito chuchu hubadilika rangi na kuwa nyeusi hali inayochochewa na homoni za mimba
13# Maumivu kwenye matiti
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata rutuba jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kufanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kuwa kawaida
14# Tumbo kujaa gesi
Utaona baadhi ya nguo zinaanza kukubana hasa sehemu ya tumbo manake homoni za ujauzito tayari zinakuwa zimeanza kutanua tumbo ,hivyo mara nyingi unakuwa unajisikia tumbo limejaa gesi
15# Kutamani kula vitu mbalimbali
Kutokana na mabadiliko yanayojitokeza ndani ya mwili yanayosababishwa na homoni za ujauzito mwanamke hujikuta akitamani kula vitu mbalimbali tofauti na mazoea yake mfano kula udongo,limao na kadhalika ili kukidhi mahitaji ya mwili wake kutokana na mzigo alionao.
16# kukauka mdomo au kuchanika
Wanawake wengine muda mfupi baada ya mimba kutunga huweza kuona mabadiliko kama mdomo kukauka sana ama kuchanika hivyo kumpa wakati mgumu hata kama akipaka mafuta huweza kukauka baada ya muda mfupi tu
17# kuumwa kichwa mara kwa mara
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kuuma kwa kichwa japokuwa si sana,hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito hata hivyo hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni zinazotokana na ujauzito.Ikumbukwe kuwa kila mwili wa mwanamke upo tofauti hivyo si dalili zote unaweza kuzipata.