Saturday, November 11, 2017

MATHARA YA KUTOKUWA KWENYE UHUSIANO WA MAPENZI MUDA MREFU


Kubali  au usikubali  kwamba kila kitu kina uzuri na ubaya hivyo hata kwenye suala la kutokuwa na mpenzi kwa muda mrefu lina ubaya na uzuri wake,leo nitaongelea upande wa mathara yampatayo mtu anayekaa kwa muda mrefu bila kuwa na mpenzi kuna mathara ya kisaikolojia yanayoweza kumpata.

1# kujikuta unajenga tabia ya kujichua (masturbation) 
Vijana wengi sana hujikuta wakikubwa na hii tabia ya kujichua ili kuridhisha hisia na miili yao tabia hii hufikia mahali inakuwa kama ulevi ambapo kuachana nayo inakuwa vigumu,vilevile ikumbukwe kuwa tabia hii inamadhara kiafya maana huwa inalegeza misuli ya uume na kusababisha baadaye unapoingia kwenye ndoa kushindwa kumtimiza haja ya mwenza wako.
2# Msongo wa mawazo
Hili linatokana na kukosa mtu wa karibu unaeweza kumshirikisha jambo lako la ndani unajikuta unatumia muda mwingi kwenye kuwaza matatizo yako  pia utakuta unashindwa kuwashirikisha marafiki zako kwa kuhofia kuchekwa hali inayoweza kushusha kiwango chako cha uchapakazi.
3# Kutojijali katika uvaaji na hata simu yako
Mara nyingi mtu akiwa kwenye uhusiano huweza kujiweka vizuri mwili wake na mavazi inapotokea unaishi pekee yako tu hali hii inaweza kupotea pia unaweza kujikuta unalalamikiwa kwa kutopokea simu mara kwa mara maana hakuna mtu anayekuweka busy na simu.
4# Ubinafsi na kufikiria nafsi yako tu siku zote
Mtu anapokuwa kwenye mapenzi huwa anajifunza kuthamini wengine kuwafikiria kuwafanya wafurahi uwepo wake na kujali hisia za mwenziwe na kadhalika hivi ndivyo kupenda kulivyo, kwa hiyo mtu anapokuwa hana mpenzi hujikuta anaanza kujifikiria nafsi yake tu,wakati mwingine hujikuta anakosa msukumo wa kujiimarisha kiuchumi.
5# Kupendelea kuangalia picha za uchi
Watu wa namna hii hujikuta wakijenga mazoea ya kuangalia picha za uchi mitandaoni ama kwenye simu zao na kuna wengine hupendelea sana kupiga chabo yaani kuchungulia watu wakiwa wanafanya mapenzi ama kusikiliza story za mapenzi.
6# Hukumbwa na tatizo la kusahau sahau na kukakamaa kwa  mgongo
Hii ni kutokana na kwamba mfumo wao wa kisaikolojia unakuwa hauko sawa ,wanawake hupendelea kudandia mambo yasiyowahusu pia kutokwa na damu nyingi waingiapo hedhini pia huweza kuingiliwa kirahisi na jini mahaba na wanaume hukakamaa migongo.
7# Kutengeneza tabia mbadala za ovyo kama ulevi
Tabia hii inakuwa mbadala wa kujiridhisha unapokuwa unataka faraja baada ya kukubwa na msongo wa mawazo hivyo ili kujiweka sawa mtu anaamua kulewa pombe ama kutumia madawa ya kulevya na bangi
8# Kutojiamini (loss of confidence)
Inafikia mahali mtu anapoteza uwezo wa kujiamini hata kuongea na watu wa jinsia tofauti na yake anaona aibu,wakati mwingine kuanza doubt mwenyewe labda anakasoro kitu ambacho kinaweza kuharibu mfumo wake wa kisaikolojia.
9# Kukumbwa na upweke
Hasa inapotokea marafiki zako wote wako kwenye uhusiano wa mapenzi kasoro wewe unajiona mpweke sana hakuna mtu wakumwelezea siri za moyo wako na hisia zako kwa kuogopa kuchekwa na marafiki wanaokuzunguka  unafikia mahali unaona kama watu wanakutenga na unawezajikuta unachukia watu wa jinsia fulani bila sababu.
10# Siku ukipata mpenzi utajikuta huna uwezo wa kutawala suala la mapenzi

Kutokana na kukosa uzoefu wa kutosha katika suala hilo utajikuta linakuchukulia muda wako mwingi kufikiria na kukufanya urudisha nyuma mambo yako mengi ya msingi,mapenzi yanaendesha sana watu wengine wanaharibu kazi sababu ya mapenzi,wengine wanajiua kisa ni hayo mapenzi hivyo mapenzi ukiyaendesha inakuwa jambo zuri ila omba yasikuendeshe utageuka  kituko mbele za watu.