Friday, September 28, 2018

SABABU KUU ZA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA / MAPENZI (KUJAMIIAANA)

Matatizo ya kufanya mapenzi au kujamiana kwa wanawake yanatambulika kama tatizo linalojirudia kwa muda mrefu ambapo huathiri mzunguko wa tendo la kujamiana (kusisimka, kufikia kilele, kurudia) na hivyo kusababisha msongo wa mawazo au kuharibu uhusiano wa mwanamke na mpendwa wake. Tatizo hili huathiri asilimia 43 ya wanawake wa rika zote duniani na huonekana sana kwa wanawake wenye umri kati ya 45-64.
Visababishi vya tatizo hili kwa wanawake ni;

  • KUSAGANA AU MAPENZI YA JINSIA MOJA KWA WANAWAKE.
  • Msongo wa mawazo – Asilimia kubwa ya tatizo hili linaweza kutokea kutokana na msongo wa mawazo ambapo huchangiwa na ugumu wa maisha (uchumi), matatizo katika uhusiano (ugomvi, kutoelewana, kutoaminiana au kukosa uaminifu katika uhusiano {infedility} nk) na magonjwa mbalimbali.
  • Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano au ndoa
  • Kujifungua mtoto – Hii ni kutokana na homoni aina ya prolactin kuwa katika kiwango cha juu wakati mama ananyonyesha, homoni hii pia hufanya kazi ya kumfanya mtu kuridhika baada ya tendo la ndoa/kujamiana kwa kuingiliana na ufanyaji kazi wa homoni/kichocheo chengine kinachojulikana kama dopamine (ambayo ndio humfanya mtu kufikia kilele wakati wa kujamiana). Mbali na kunyonyesha, homoni ya prolactin pia huongezeka wakati mtu amelala (usingizi mzito au REM sleep), wakati wa alfajiri, baada ya kufanya mazoezi, kula,baada ya tendo la kujamiana, baada ya upasuaji mdogo na hata baada ya kupata degedege. Sababu nyengine ya kuongezeka kiwango cha kichocheo hiki cha prolactin ni kuwa na saratani katika ubongo (anterior pitituary tumors). Dalili za saratani hii ni pamoja na kutonyonyesha vizuri kwa mama, kukosa hedhi, ugumba kwa wanawake na uhanithi kwa wanaume(impotence).
  • Kupungua mzunguko wa damu katika tupu ya mwanamke na hivyo kusababisha maumivu wakati wa kujamiana.
  • Hypothyroidism – Matatizo ya homoni ya tezi la koo, huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume.
  • Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi au vya majira kwa muda mrefu
  • Unywaji pombe kupindukia – Kinyume na fikira potofu za watu wengi ambao huamini kwamba unywaji pombe kali huongeza hamu ya kujamiana au kupunguza uzito lakini ukweli ni kwamba pombe kali au kilevi cha aina yoyote hupunguza hamu ya kujamiana na pombe huongeza uzito na kusababisha utapia mlo.
  • Ugonjwa wa kisukari
  • Uvutaji sigara
  • Ujauzito – Kutokana na mabadiliko katika mfumo wa homoni au vichocheo wakati wa ujauzito, na pia kutokana na mabadiliko ya maumbile ya wanawake wakati huu na hivyo kuchangia kutojiamini kwa mwanamke.
  • Uzito uliopitiliza (obesity)
  • Ugonjwa wa mifupa (arthritis)
  • Utumiaji madawa ya kulevya
  • Madhara katika neva inayohusika na kuongeza msisimko wakati wa kujamiana (pudendal nerve damage) wakati wa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kwa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi au katika mfuko wa kizazi.
  • Madhara ya dawa – Kama dawa za kutibu shinikizo la damu,antidepressant medication, dawa za saratani nK.
  • Uchovu – Kuzidiwa kwa mwanamke na majukumu ya kulea mtoto/watoto, kazi na kumhudumia mume wake hivyo kusababisha uchovu.
  • Ugonjwa wa moyo
  • Saratani ya aina yoyote ile
  • Kuwa na wasiwasi (anxiety), depression nk.
  • Historia ya kubakwa, au kupata maumivu wakati wa kujamiana hapo awali kutokana na mwanamke kutokuwa tayari kujamiana au kutotayarishwa vyema kabla ya kujamiana au magonjwa ya zinaa.
  • Tatizo la vaginismus – Hii ni tatizo ambalo husababisha tupu ya mwanamke kuwa ndogo wakati wa kujamiana na hivyo husababisha mwanamke kupata maumivu wakati wa kujamiana.
  • Kupenda intaneti kupita kiasi (addiction) – Katika tafiti mpya iliyofanyika mwaka huu nchini marekani, imeonyesha ya kwamba kati ya ndoa 6,000 zilizovunjika asilimia 57 zimesababishwa na mwenza mmoja au wote kupenda kuchat au kutumia intaneti kupita kiasi na hivyo kusababishwa msisimko kupotea kati ya wenza wawili na hatimaye mwisho ni kupungua uwezo au hamu ya kujamiana.
Ni kundi gani la wanawake lililo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili?
  • Wanawake ambao wana historia ya kupungua hamu ya kujamiana
  • Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali
  • Wanawake ambao waliofika umri wa kuacha kupata hedhi (menopause- miaka 42-58)) na kupata dalili mbalimbali kama kutokwa na jasho usiku, kukosa usingizi mzuri nadepression.