Wednesday, November 1, 2017
HATIMAYE WANAUME KIBAO KIMEWAGEUKIA
ilishazoeleka toka enzi za mababu wanawake kunyanyaswa katika mahusiano, wanawake enzi hizo walikuwa wanalia sana na wakuwabembereza hakupatikana. naweza kuamini pengine wanawake walisali wakakesha kwenye nyumba za ibada ili waepukane na manyanyaso katika mahusiano. ilikuwa ni jambo la kawaida sana kukuta mwanamke analia huku kabeba mtoto mgongoni na furushi la mizigo ya nguo zake eti mume kamfukuza...
ni kama kilio chao kimesikiwa kwani siku hizi wanaongoza kwa kulia na kunyanyaswa kwenye mahusiano ni wanaume/wavulana siku hizi wanawake wameelimika sana tofauti na enzi hizo, siku hizi wanawake wanajimudu kifedha mvulana/mwanaume ukimzingua anatembea mbele kwa mbele...siku hizi wanawake nao wanaoa wanaume, wanaume wanalelewa na wanawake sasa chunga sana ukikosea mwanaume unatimuliwa kama mbwa...enh kibao kimetugeukia si kutesa kwa zamu, sasa ni zamu ya wanawake nao kutesa...
wanawake siku hizi nao wanafanya mazoezi ya mwili hasa yale ya mchezo wa ngumi, ili kupambana na mwanamke wa siku hizi lazima mwanaume ujipange lasivyo anaweza akakuadhibu ukachanganyikiwa wanawake wanapiga sana siku hizi, siwasifii maana ila baadhi ya wavulana wanakiona cha moto kutoka kwa wanawake waliokulia nzega...nadhani kutokana na mioyo yao kuumizwa sana na wao wamejikita kwenye utafutaji wa fedha ili waweze kujikimu.
wanawake siku hizi wana pesa chafu cheki mjengo wa beyonce juu hapo....mtu kama huyo si anaweza kuoa mwanaume yeyote anaemtaka...hivyo wanaume tuamke tusake pesa, tuache tamaa za kulelewa na wanawake maana mwanamke anataka kujifanya anakulea ili mwisho wa siku aje akuumize akunyanyase na akufukuze kulipa machungu ya tulichokuwa tunawafanyiwa...wanawake walinyanyasika wewe pia ni shahidi hivi sasa ata kesi za fulani kampiga mama fulani zimepungua kabisa...enh mwanaume atampigaje msichana wakati ndie anaemuweka mjini...
hivi sasa kuwe na mashindano ya mali, magari na majumba ila kusiwe na mashindano ya vilio vya mapenzi, wanaume tukizembea wanawake watatuacha sana kimaisha...tufanye kazi kwa juhudi kukabiliana nao tuwe na pesa tuoane kila mtu akiwa na pesa zake mkizinguana kila mtu anachukua hamsini zake kimya kimya naamini vilio vya mapenzi vitapungua...ila mvulana akiwa na pesa msichana hana ni shida na manyanyaso...vile vile kwa msichana akiwa na fedha mwanaume utanyanyasika sana...utalia na kusaga meno...ila mbinu rahisi ni kuamua kufanya kazi kutafuta fedha kama mwendaazimu ili baadae tuje tuyafurahie mahusiano...najua mtaidharau hii post baadhi ila hayo ni maoni yangu binafsi...