Kila mwanaume aliyekwenye uhusiano hupenda kujua hali ya uhusiano wake,hupenda kujua kama mwanamke aliyenaye anampenda kweli ama hana mapenzi ya kweli kwake! Ni muhimu kujua kama mapenzi uliyenaye ni chaguo sahihi kwako,Leo msomaji wangu wa maishahalisi blog napenda nikupe namna ya kumtambua mwanamke mwenye mapenzi na wewe.pia tazama sifa za mwanamke anaefaa kuolewa
1# Dadisi kujua kitu gani anapenda kutoka kwa mwanaume kama ni pesa,umaarufu,power ama mvuto wa asili
Jibu lake litakupa mwanga kuweza kujua mawazo na namna anavyowaza juu ya uhusiano na kukuonesha kama kilichomvuta kwako ni pesa,hadhi,tabia ama mapenzi asilia,ifahamike tu kwamba kama mwanamke hana mapenzi ya kweli kwako lazima kuna kitu kingine tu ambacho kinamfanya awe na wewe kuwa makini.
2# Muulize kuhusu sababu zinachomfanya akupende
Swali hili ni la kawaida ila litakupa dalili nyingine yakumpima,kama atajibu swali hili bila kufikiri kwa muda wala kupepesa macho huyu atakuwa anakupenda kweli,kama akianza kupepesa macho na kufikiria kwa muda kama mtu anayepanga kitu cha kukujibu hapo kuwa making hiyo anaweza kuwa ni tapeli tu anapanga namna ya kukufurahisha tu.
sifa 5 za wanawake ambao hawaolewi
3# Je, yupo tayari kukutambulisha kwa wazazi,marafiki ndugu na jamaa zake?
3# Je, yupo tayari kukutambulisha kwa wazazi,marafiki ndugu na jamaa zake?
Mara nyingi utambulisho wa kimahusiano hasa kwa wazazi huwa ni jambo ambalo huwa halina mzaha,ili kujua mtu ambaye amejitoa kweli kwako unaweza kumwomba akutambulishe kwa wazazi kama atakuwa tayari bila kusita ni dalili ya kukukubali.
4# Je anajisikiaje unapomgharamia Mara kwa mara
Mpe zawadi na Mtoe out Mara kwa Mara na usubiri wakati wa kulipa bill umchunguze vizuri je , anaona aibu au anakosa kujiamini kwa sababu Mara kwa Mara wewe ndo unamlipia bill hii ni nzuri hasa kama uhusiano wenu utakuwa umeanza kama marafiki tu.kwa mtu anayekupenda kweli hapa lazima aoneshe kutojisikia vizuri wewe kila mara kulipia bill ya chakula mnapokuwa out au mpeleke shopping alafu nguo nzuri anazozipenda jifanye kuwa ni ghari mno kuzinunua kwa kuwa bajeti yako hairuhusu mchunguze uone anajali kwa kiwango gani ni rahisi kumtambua kama ni mbinafsi kwa kujijali matakwa yake tu bila kuangalia upande wako pia
5# Chunguza kama anakumbuka matukio muhimu kwako kama siku yako ya kuzaliwa
Kwa mtu anayekupenda kwa dhati na yule hasa anayejufikiria na kukuona were ni sehemu ya maisha take ni rahisi kushika kichwani baadhi ya vitu vinavyokuhusu mfano kujua namba yako ya simu kichwani,Sikh yako ya kuzaliwa na vitu vingine vinavyokuhusu kama hayuko hivyo kaa nae makini
6# Anajisikiaje anapokuona huna amani?
Mwanamke anayekupenda na kukujali hayupo tayari kukuona ukiwa huna amani,umenyong’onyea,huna raha alafu yeye akaendelea kuwa kufurahi tu lazima naye atspoteza furaha take kwa kukuona were hauko sawa na ikibidi atapenda kujua kitu gani kimekusibu mpaka use mwenye simanzi namna hiyo.
7# Je, anafurahia uwepo wakinaruhusu
mke mwenye mapenzi ya kweli utamjua tu pale unapokuwa nae kama anafurahia uwepo wako ama la, wanawake wengi hujikuta ni watu wenye kutabasamu tu mara nyingi unapokuwa unaongea nae hata kama unachokiongea si kitu cha kufurahisha ila huonesha kufurahia maongezi ,kuna ule muda mnaonana mahali hata kama anaharaka atajikuta amechelewa bila kutarajia.mambo 10 yanayopelekea ndoa kuvunjika
8# Je, anajitolea muda wake kwa ajili yako?
Muda ni Mali,muda unathamani yake Mara nyingi huwa tunajikuta tumebanana na majukumu ya hapa na pale huku Siku zikizidi kusonga ila hata katika mbanano huo kwa MTU mwenye mapenzi ya kweli lazima atajaribu tu kupata muda walau kidogo wa kuonana na kuongea na mtu ampendae kwa dhati ila kama siyo MTU mwenye mapenzi ya dhati hataweza kukupa muda hata kama ratiba take inaruhusu Tazama pia ukiwa kwenye mapenzi vitu hivi utakutana navyo