Saturday, November 11, 2017

TATIZO LA KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA

Tatizo hili hutokea kwa baadhi ya wanaume ambapo anapata msisimko mapema au mara tu anapoanza tendo la ndoa na kumfanya amalize muda huohuo, yaani muda usiozidi hata dakika tatu. Tunaposema kamaliza tendo ni kwamba anafikia kilele au mshindo na kutoa manii.
Wanaume wenye hali hii wakati mwingine hutoa manii hata kwa msuguano mdogo endapo ataguswa au kugusana na mwanamke na akijenga hisia hata kwenye msongamano atajikuta tayari ameshachafua nguo. Ukifikia katika hatua hii basi upo katika hali mbaya.
Ingawa tunasema kuwahi kumaliza ni chini ya dakika tatu, lakini kuna baadhi ya tafiti zinasema kuwahi kumaliza ni pale unapotoa manii ndani ya dakika moja au sekunde kumi na tano kwa baadhi ya tafiti.
Wanaume wanaowahi kumaliza mara nyingi hulalamika kushindwa kujizuia kudhibiti utoaji wa manii na hujikuta zikitoka zenyewe na wanakuwa hawafurahii tendo wala wenza wao pia hawafurahii. Tafiti zinaonesha kuwa hali hizi zinatofautiana kati ya mwanaume na mwanaume.
Kwa kawaida kabisa, mwanaume hadi kufikia kileleni yaani kumaliza tendo la ndoa inatakiwa atumie dakika nne hadi nane, chini ya dakika nne ni tatizo na zaidi ya dakika nane siyo mbaya kama ataweza kijidhibiti mwenyewe.
Wanaume wengi wenye tatizo hili hulalamika kuwa na msongo wa mawazo kutokana na masuala mbalimbali ya kijamii, mfano matatizo katika uhusiano wa mapenzi, kazi na mengineyo.
Hali hii inaweza kukujengea woga wa kuogopa kufanya tendo la ndoa au hata kuwa na uhusiano na mwanamke. Mwanaume akiwa anawahi kumaliza tendo, mwanamke hadhuriki moja kwa moja bali huathirika kisaikolojia kwa kuwa anashindwa kufurahia tendo na yeye kufikia kileleni.
CHANZO CHA TATIZO
Hadi sasa chanzo halisi cha tatizo hili bado hakijulikani lakini utafiti unaonesha kwamba watu wenye historia ya kujichua ‘Masterbation’ wakati wa umri wa balehe na ujana ndiyo wanaoathirika zaidi na tatizo hili.
Tatizo lingine ni woga au wasiwasi unapofanya tendo, hali iitwayo kitaalamu ‘Performance anxiety’. Hii inatokana endapo unafanya tendo hilo kwa kuogopa aidha kufumaniwa au una wasiwasi na mpenzi wako juu ya magonjwa au mimba, basi kila mara ukiwa hivyo una hatari ya kupatwa na tatizo hili.
Endapo ulikuwa na matatizo katika masuala ya mapenzi kwa hiyo hujayamaliza na mwenzio na unafanya tendo basi tu kwa lengo la kutimiza wajibu, pia ni mojawapo ya chanzo cha tatizo.Kutofanya tendo la ndoa mara kwa mara yaani unakaa siku nyingi, hivyo siku unajaribu kufanya tendo hilo unajikuta unawahi kumaliza.
Yapo matatizo mengine ambayo pia ni chanzo cha tatizo. Matatizo haya zaidi ni ya kifiziolojia. Nayo zaidi huhusiana na matatizo katika mfumo wa homoni au vichocheo mwilini hasa homoni ya ‘Serotonin’.
Itaendelea wiki ijayo.