Friday, July 13, 2018

SIFA 10 ZA MWENYE MAPENZI YA KWELI . .

Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada. 

*      Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .

*      Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri

*      Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.

*      Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima.

*      Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)

*      Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine,hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.

*      Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.

*      Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .

*      Atakuwa tayari kuvumilia,hatak uwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.