Sunday, November 19, 2017

Epuka Kumsifia Mwnaamke Mwingine Mbele Ya Mpenzi Wako, Acha Kutaka Vitu Mabavyo Hana

Kama ambavyo wanaume hawapendi kusikia kuhusu wanaume wengine ndivyo hivyo ambavyo wanawake hawataki kusikia unasifia wanawake wengine, wawe wapiti njia, marafiki zake au hata wale unapowaona kwenye TV. Pale utakaposifia kuwa “yule muigizaji anakifua kizuri” itakuwa ni sawa na umemuambia mpenzi wako anakifua kibaya na angalau kwa wanaume ni rahisi kusahau lakini kwa mwanamke kila wakati akimuona yule mwanamke au mwanamke aliyefanana fanana na yule hata kama ni kwenye TV atajisikia vibaya sana.
Wakati mwingine atahisi unamsaliti na hatajiamini. Kwakifupi acha kusifia mwanamke mwingine mbele ya mpenzi wako, acha kujifanya unasema mimi napenda wanawake wa aina flani…to hell na wa aina flani, kama umemchagua huyo inamaanisha ndiyo aina ya unaowataka. Unapata faida gani kumfanya mwenza wako kujisikia vibaya kutokana na muonekano wake.
Unaweza kumuambia “Baby napenda uwe unavaa nguo za aina flani, zinakupendeza na nazipenda… Hiyo ni sawa kwakuwa nguo anaweza enda shona dukani na akawa kama unavyotaka, lakini hana tako unamuambia unataka matako, chuchu saa sita unamuambi unataka sijui makubwa ya kushika…yeye ayapate wapi, ungetaka ungewafuata wanye hivyo vigezo.

Umemkuta na unene wake wa asli unamuambia unataka slim, unamsumbua dada wa watu kujikondesha kumbe ndiyo alivyo zaliwa na hapungui. Anajilazimisha kula malimau na kushinda njaa kisa ufurahi! Kwa mwanamke muonekano wake ni kila kitu, akihisi hufurahii muonekano wake jua kuwa hata kitandani hatafurahia, hutamridhisha na kubwa kabisa hata wewe unaweza usiridhike na huo ukawa mwanzo wa kuvunja uhusiano wenu, chagu cha kuongea na wakati wa kukiongoa.