Thursday, July 19, 2018

POSITION ANAYOTAKIWA KULALA MAMA MJAMZITO.

Mama anapomaliza first trimester  (miezi 3 ya mwanzo) tumbo linaongezeka ukubwa kutokana na ukuaji wa mtoto. Ukuaji wa mtoto unadhiri pisition ya ulalaji wa mama,hivyo mama anashauriwa mimba ikifika miezi 4 (wiki 16)asilalie tumbo au mgongo.

MAMA ASILALIE TUMBO AU MGONGO
Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi ya mishipa ya mgongoni  inayosafirisha damu kutoka kwenye uti wa mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani  kushindwa kusafirisha damu vizuri  na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu  unaoweza kumuadhiri mama au mtoto.


Adhari atakazo zipata mama mjamzito atakapo lala kwa mgongo (chali) / kulalia tumbo

Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama,

:Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono)

:Kushuka au kupanda kwa blood pressure

:Ini kuelemewa uzito

:Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto

:Kusikia kizunguzungu mara kwa mara

:Mama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku

:Kukoroma

:Maumivu ya mgongo

:Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen)

:Mtoto kukosa virutubisho vya kutosha.



Mama anatakiwa alalie position gani ili awe salama?

Tafiti nyingi zinamshauri  kwamba mama mjamzito alalie upande wa kushoto .Sababu damu husafirishwa kwa  Urahisi zaidi kutoka kwenye moyo wa mama na kwenda kwenye kondo la mtoto  na kumpa virutubisho vingi zaidi.  .


Iwapo mama atalalia tumbo au mgongo ifamfanya mtoto asiwecomfortable  atahangaika na kumpiga piga mama ili abadili position ya kulala.


USHAURI

Mama anapolala ni vizuri akaweka mto katikati ya miguu usibane miguu ipitanishe, inakusaidia kulala comfortable,damu kusafirishwa vizuri na kutopata maumivu ya mgongo.Nyakati za usiku ni kawaida kwa watoto  kupiga piga tumboni ,ila akipiga sana jua umelala vibaya anataka ubadilishe position.