Saturday, October 28, 2017

UFAHAMU UGONJWA WA FANGASI ZA SEHEMU ZA SIRI NA MATIBABU YAKE.[CANDIDIASIS]

ugonjwa wa fangasi za sehemu za siri husababishwa na aina ya wadudu wa fangasi kwa jina la candida albicans.
fangasi za uke hupenda kuwashambulia wanawake ambao wako kwenye umri wa kubeba mimba lakini pia sababu yeyote inayosababisha kinga kushuka huachangia mashambulio ya mara kwa mara ya ugonjwa huu mfano mlo mbovu, ugonjwa wa kisukari, kansa na ukimwi, ujauzito matumizi ya mda mrefu wa dawa antibiotic na dawa za steroid yaani jamii ya predinisolone na hydrocortsisone.
ugonjwa huu hauambukizwi kwa njia ya ngono na maambukizi kwa mwanamke haimaanishi kwamba mwanaume lazima atibiwe au maambukizi kwa mwaume haimaanishi mwanamke lazima atibiwe kama ilivyo kwenye magonjwa ya zinaa.
mara nyingi mgonjwa anayeugua mara kwa mara fangasi hata kama sio za uke ni dalili kwamba kinga imeshuka hasa kwenye ugonjwa wa ukimwi.

                                                 dalili za fangasi za sehemu za siri
  • miwasho ya sehemu za uke.
  • kutokwa uchafu wa rangi ya maziwa ukiwa haina harufu kabisa au harufu ya mkate kwenye uke.
  • sehemu za uke kuvimba na kua nyekundu.
  • maumivu ya kuungua wakati wa kukojoa kwa wanawake.
  • maumivu wakati la tendo la ndoa kwa wanawake.
  • kwa wanaume, wekundu na wakati mwingine kutokwa na uchafu kidogo kwenye uume.
                                            vipimo vinavyofanyika

        mara nyingi daktari huweza kuutambua ugonjwa huu kwa dalili tu bila kupima lakini wakati mwingine kiasi cha uchafu unaotoka hupimwa kuhakikisha hakuna ugonjwa mwingine wa zinaa ulioambatana na fangasi.
vipimo kwa kutumia darubini huonyesha fangasi kwa mgonjwa.
                                                      matibabu
  •  cotrimazole vidonge, chomeka kwenye uke kidonge kimoja cha 100mg mara moja wakati wa kulala kwa siku saba.
  • cotrimazole ya kupaka 1%, paka asubuhi na jioni kwa siku 7 mpaka 14.
  • grusiofulvin vidonge vya kumeza kimoja kila siku kwa wiki mbili na  kama dawa hizo zikishindwa meza flucunazole kidonge kimoja kila siku kwa siku 14.
                                                    jinsi ya kuzuia
  • acha sehemu za siri safi na kavu muda wote yaani epuka kuvaa nguo za ndani kabla hazijakauka.
  • epuka sabuni kali za sehemu ya siri, marashi ya kwenye uke na kuingiza vidole mara kwa mara kuosha uke.
  • badilisha tampoon mara kwa mara.
  • vaa nguo za ndani zilizotengenezwa na pamba na sio nailoni.
  • kama una kisukari hakikisha sukari yako iko vizuri na kama una virusi vya ukimwi basi meza dawa na kufuata masharti yote ili kinga yako isishuke.
  • kula mlo kamili yaani wanga, protini, matunda na mboga za majani kuweka kinga vizuri.