Monday, November 13, 2017

Furaha sio kile ulichonacho, bali ni kwa kiasi gani unafurahia maisha.

Furaha ya kweli inaletwa na wewe peke yako.Wengi wetu huwa tunaamini kwamba kadiri tunavyozidi kuwa na vitu vingi basi ndivyo furahara inazidi kuongezeka maishani mwetu. Lakini swali ni Je swala hili lina Ukweli wowote?
Kadiri tunavyozidi kukua kiuchumi, ndivyo tunavyo onekana tukiishi maisha bora zaidi. Tunapata Fedha zakutosha kununulia yale mambo yote tuliyowahi kutamani kuyamiliki hapo mwanzoni na maisha yanasonga kwa namna hiyo. Laki swali jingine linakuja hapa kwamba, Je mambo haya yote tunayomiliki yataweza kutupatia Furaha ya Kudumu??
Kuna muda labda ulikua ukihifadhi fedha kwa ajili ya kununua kitu cha thamani kama vile Simu, Gari la kifahari n.k na mara baada ya kununua kitu kile, Furaha huongezeka zaidi lakini furaha ile hupungua mara baada ya Mwaka, Mwezi, Wiki na hata siku kwakua tuu kitu kile ulichonunua kitakua teyari kimekwisha poteza Mng’aro wake na mvutu hivyo basi hakitakupendeza tena machoni mwako na utalazimika kutafuta kingine na hapo ndio furaha hupotea tena.
Ukweli ni kwamba, Tunaweza tukawa tuna miliki mali na vitu vingi kuliko hata vizazi vilivyo pita, lakini hatuna furaha kama tunavyo-paswa kuwa na Furaha.
Kuna uwezekano wa sisi kuwa tumekwisha anguka katika mtego ambao hutufanya sisi kukaa mbali na Furaha ya Kudumu ambayo tumekuwa tukiitafuta katika kipindi chote cha Maisha yetu. Angalia kama umeanguka katika mitego hii mitatu(3) kisha ujue ni kwa namna gani utaweza kujinasua katika mitego hivyo.

Tunafanya kazi kwa bidii lakinu tunajikuta watumwa wa Matamanio.

Kuna aina ya watu ambao wao hufanya kazi ama kitu kwa bidii ili kuridhisha nafsi zao(Kwa lugha ya kiingereza wanaitwa hedonist). Hedonist ni yule mtu anayepambana kwa kadiri awezavyo ili kuhakikisha anaipoza nafsi yake huku akisau upande wa pili(Madhara) ya yale mambo afanyayo ili kuipoza nafsi yake. Huangali upande mmoja ya Starehe na kusau upande wa pili ambao ni Maumivu. Ni jambo la kawaida sana kwa watu hawa kubaki kuwa watumwa wa matamanio kwakuwa tuu Furaha watakao ipata ni ile ya muda mfupi ambapo baada ya hapo watarudi tena katika huzuni.

Tunafanya kazi lakini tunateseka kwa maumivu.

Mtego huu ni kinyume cha ule mtego alioko Hedonist. Mtego huu ni kwamba mtu anafanya kazi kwa nguvu zake zote akiwa na matumaini ya Kuipata furaha katika matunda ya kazi hiyo anayofanya. Anasahau maumivu anayopata kwa wakati alioko  na kupata faraja kwa matunda yajayo mbeleni. Jambo hili halina maana yeyote kwa wakati huu zaidi ya kutumia muda mwingi ili kupata mazao mema hapo baadae, jambo ambalo huondoa kabisa Furaha mioyoni mwetu licha yakua na matumaini kwa kile kijacho.

Hatufanyi chochote kwa bidii lakini tunapoteza shauku na matarajio ya baadae.

Wakati mwingine unaweza ukafikiri ni bora kutofanya juhudi ama kufanya kazi kwa bidii. Ingawaje unapoamua kuwa mtu wa kuona maisha hayana maana(nihilist) kuna weza kukakupa guarantee ya kupata furaha ya kudumu. Ukiwa katika halii hii ya kuona maisha hayana maana ni hatari sana maana utashindwa kuenjoy maisha ya sasa na hata kupoteza tumaini kwa maisha yajayo.
Tunatumia miaka mingi kuishi maisha yetu katika ulimwengu huu na itakua ni sawa na taka kama hatutaweza kujaribu kile kinachoitwa Furaha ya kweli. Rahisi Kuja na ni rahisi Kupotea.
Yapo mambo mengi tunayoweza kufanya ili kuipata furaha itakayoweza kudumu kwa muda mrefu.

1.Piga picha na tunza kumbukumbu ya matukio yote chanya yaliyogusa hisia zako.

Kwa kuliweka swala hili kiurahisi zaidi, Kadiri unavyotuza kumbukumbu za matukio yalioguga Hisia zako(Hisia chanya), basi ndivyo kadiri furaha yako inavyozidi kudumu. Wanasaikolojia wanasema hisia chanya hujumuisha Furaha, Hali ya kushukuru(gratitude),Upole, matakwa, Tumaini, hamasa,na upendo. Hisia hizi chanya kwa pamoja hutufanya sisi kuwa vyema kiakili na kifikra na hata miili yetu kunawiri.
Jaribu kukusanya matukio hayo yote na kuyatunza katika diary ama katika simu zetu kuliko kutunza matukio ambayo hayaendani nasi ambayo kwa namna moja ama nyingine huja kuondoa ile furaha tuliyokuwa nayo hapo awali. hii itakusaidia sana kuitunza ile Fura uliyokuwa nayo hapo awali.

2.Jikite zaidi katika kile unachokifanya.

Wasafiri pasipokua na malengo siku zote furaha hutoweka. Wasafiri wa aina hii hujaribu kutenganisha muunganiko ulioko Duniani huku wakitoa visingizio vya hapa na pale. Wako njiani lakini hawajui wanaelekea wapi.

Lakini badala yake, Lakini katika maisha yetu ya kila siku kama tutawekeza vilivyo katika vile tunavyofanya ama kusema, basi lazima Furaha itatuzunguka. Kujikita zaidi katika kile unachokifanya kutakufanya wewe kuacha kushangaa na kujiuliza maswali mengi ambapo yatakupa msongo wa mawazo huku furaha yako ikitoweka. Matokeo chanya ya kile kitu ulichojikita kukifanya siku zote hukupa faraja na matumaini tele kwamba maisha yako yana maana na ndipo Furaha yako Huja pasipo kikomo.

3.Tohoa maana katika kila kitu unachofanya.

Kama tunashindwa kupata maana katika kile tunachokifanya, tunakua tuu tukikumbatia hisia za kukosa mwishoni tunaanza kuona kwamba tunapoteza Muda wetu na nguvu zetu. Ifike pahala sasa tusiwe kama wafanyavyo nihilists yaani wao wanaonaga maisha hayana maana kabisa.
Kusema kweli, kuna mambo mengine hutukwaza na kuona kwamba maisha haya hayana maana lakini ukweli ni kwamba ndani ya Vitu hivyo ndipo Furaha ya Kudumu tunapoipata. Jitahidi kutafuta maana katika vitu hivyo, na vichukulie kwa mtazamo chanya kabisa na unapokua unakosa mpinzani katika jambo hili basi itakua rahisi sana kwako kushinda lakini unapokupata upinzani mkali na kushindwa kuhimili upinzani hu, itakua ni nafasi ya wewe kushindwa na mwishoni kupotea na Furaha kwako ukaisikia tuu kwa wengine.

4.Jenga Mahusiano bora na wengine.

Kuna wakati fulani tunahitaji connection fulani fulani ili mambo yaende sawa. Connection kutoka kwa marafiki, Familia ama hata wapenzi zetu. Lakini tunachofaidika katika mahusiano hayo sio KIASI(QUANTITY) bali ni UBORA(QUALITY).
Kuna wakati wote kwa pamoja mnaweza kunufaika na Mahusiano hayo lakini ni kwa mara chache sana. Kuwa na mahusiano Bora ni hadithi nyingine kabisa kwani hutufanya sisi kufunguka bila kuogopa chochote. Mnabadilishana mawazo kwa chat za hapa na pale hii yote ikiwa tuu wewe unapata support kihisia na mwenzako pia hivyo hivyo.There is nothing better than being deeply known by someone who knows you better than yourself and speaks your mind.