Thursday, July 19, 2018
CHOMBEZO; STORI TAMU YA KUSISIMUA SITA KWA SITA 04
"Hallo ! Mambo Osward " aliongea Fifi baada ya kuwa Osward amepokea "Poa , Nambie Malaika " "Hahahah acha utani Osward , Mimi naweza kuwa Malaika au unanijaza tu " Aliuliza Fifi "Kwanini usiwe tena unaweza kuwa zaidi hata ya Malaika " "Mmm haya Ahsante , Vipi lakini ?" Aliongea Fifi huku akiusogeza mto na kuuweka mapajani pake na kuugemea "Shwari tu , ndo nilikuwa najiandaa hapa nilale nikajua huto nipigia " aliongea Osward "Siyo rahisi , kuna kazi nilikuwa namalizia kidogo , baada ya kumaliza nimeingia kuoga ndo nikasema ngoja nikupigie nisingeweza kuacha kukupigia" aliongea Fifi "Poa nambie " "Amm kesho tunaweza kuonana pale Calabash saa nne asubuhi ? " aliuliza Fifi "Keshooo !! .. Poa Kesho sina kipindi nadhani itawezekana na hata Kama ningekuwa nacho lazima ningekuja kuonana na wewe Malaika " aliongea Osward huku akitia mikogo na kujifanya anajali jali kumbe ana lake tu jambo "Hahaha Osward bhana unaonekana mcheshi Sana Eee" "Hapana ila niukweli ambao nashindwa kuuzuia kwanini niongope ikiwa moyo na macho vimeona" "Mm haya bhana , nikutakie usiku mwema na pole Kwa kuisubiri simu yangu "
"Usijali , Nawe pia Malaika "
Baada ya kumaliza maongezi na kutakiana usiku mwema Fifi akakata simu na kujilaza kitandani huku simu yake akiwa ameiweka kifuani akifikiria namna ambavyo ataanza kumweleza Osward hisia zake kumbe hajui Osward nae anafikiria nini juu yake
Palipo pambazuka mida ya saa tatu asubuhi Osward Kama kawaida yake Mzee wa kuazima nguo akazama chimbo kwa washikaji zake na kuweza kuazima nguo akajipigilia ile ile na kujimwagia unyunyu huku shingoni akiwa amening'iniza vicheni uchwara Kama vinne ivi halafu vyote feki alipoona amekuwa tayari alianza kusogea taratibu akiwa Kwa miguu kwani kutoka Sinza anapokaa na ilipokuwa Calabash Restaurant hapakuwa mbali hasa kwa wale wenzangu na Mimi ambao nauli kwetu ni za bajeti basi huwa hatuoni shida hata kutembea kutoka ubungo mpaka Kariakoo
Osward alipofika aliingia moja kwa moja mpaka ndani na kwenda kuketi "Kaka karibu " alikaribishwa na Dada mmoja mhudumu wa pale "Aam , Naomba maji kubwa moja moto na ice cube " aliagiza Osward na yule Dada kwenda kufuata na kumletea "Karibu " "Ahsante , samahani sijui unaitwa nani mrembo " aliongea Osward "Naitwa Teckla" alisema Teckla huku akijichekelesha chekelesha "Teckla unajua kuwa wewe ni mrembo ?"
"Mm Ahsante " aliitikia Teckla huku akipepesa macho yake pembeni kwa kuona aibu "Naweza kupata namba yako ya simu tuwe tunawasiliana " "Bila shaka "
Osward alilitoa lisimu lake lile la tachi lililopasuka kioo
"Aaa Jana wamenipamia simu yangu nilikuwa nashuka wenye gari ikaanguka aisee hapa kioo kimepasuka hatari , Mijitu mingine inatuingizia gharama ambazo hazipo kabisa na usawa huu wa anko Magu ( Osward akajisemelesha mbele ya Teckla baada ya kuitoa simu ) .. Enhee! 07... " "65241xxx" Teckla aliimalizia "Poa , Ahsante ntakutafuta "
Osward baada ya kuisevu namba ya Teckla akairudisha simu mfukoni Mara kwa nje akaona kuna gari ndogo nyeusi aina ya Spacio na kuweza kuteremka msichana Fifi kisha akatoa simu yake na kuweza kumpigia Osward "Hallo ! Osward Nimeshafika umekalia kwa wapi ?" Ilikuwa ni sauti ya bidada Fifi baada ya kuwa Osward amepokea simu "Nakuona we ingia ndani huku mwisho utaniona " aliongea Osward
Fifi akakata simu na kuanza kusogea taratibu akiangaza huku na kule na kufanikiwa kumwona alipokuwa amekaa Osward na kumfuata
"Ooh! Mambo " Fifi alitoa salamu na kumpatia mkono wake Osward "Poa karibu " "Ahsante , Samahani sana kwa kuchelewa kulikuwa na foleni kubwa "
"Wala usijali , Nambie uko poa lakini "
"Yah ! Vipi mbona umeagiza maji tu peke yake hutumii vinywaji vingine " "Natumia ila kwa Leo nimependa nitumie maji "
"Mmmm ya kweli hayo au unanionea aibu ila ukiwa peke yako unakunywa " "Hahahaha hapana kwanini nikuonee aibu wakati bia nacho nikinywaji cha kawaida hakina utofauti na maji "
Wakati wanaongea Teckla alifika na kumwuuliza Fifi atatumia nini "Aaam nileteee! Coca cola ya baridi ya take away moja " "Sawa "
"Osward uagizi chakula ?" Aliuliza Fifi "Mm hapana nimeshiba sana sina hamu ya kula kabisa " "OK, Dada niletee Coca cola tu chakula hapana "
Teckla aliondoka na kwenda kufuata kisha kumletea .