Tuesday, May 8, 2018

ALAMA 5 ZITAKAZOKUONYESHA KUWA MPENZI WAKO HAKUHESHIMU TENA

"Wakati wanawake wengi wanatamani upendo, wanaume wengi wanatamani heshima . Baadhi ya wanaume hawajui hata heshima ya mwanamke ikoje kwa sababu ya kutokuheshimiwa na wapenzi wao""


Wanaume wengi Wanafikiri kuwa kuwa na mpenzi ambaye anapiga magoti akiwa anasalimia,kupika au kumtengea vyakula vitamu mezani kama alama ya heshima.Mara zote wanawake watafanya mambo kama haya kwa sababu wanahitaji kitu flani kutoka kwako,lakini kusema ukweli hatakuheshimu kama mwanaume.Hizi hapa ndizo alama ambazo ukiziona tu mpenzi wako anazo basi ujue hakuheshimu kabisa.


1.Hakupongezi kwa lolote:Mwanamke anaye kupenda atakubali kazi yako unayoifanya na atakupongeza na kukupa pole kwa kazi ngumu unayoifanya pale unapofanikiwa anazidi kukupa moyo na kukushauri ili ufanikiwe zaidi.Wakati huo utagundua namna anavyotabasamu juu yako na anavyo ongea,kwa sababu anakuwa anafurahi kuwa na wewe.Lakini kama mwanamke anakuzarau hutaona pongezi yoyote sana sana akijitahidi utaona anafosi kucheka lakini kunakuwa hakuna furaha kutoka moyoni kuwa makini sana kunakitu kinakosekana.

2.Anakusema anapokuwa na watu wengine:Ni alama kubwa sana ya utovu wa heshima
kama mpenzi wako hana kitu kizuri cha kusema kuhusu wewe anapokuwa na marafiki zake au familia yake,anaweza akajifanya anasema mambo mazuri pale wewe unapokuwa upo,lakini mara tu unapogeuza mgongo hana kitu lakini maovu tu ndiyo atakayoyasema kwa yoyote yule ambaye yuko tayari kusikiliza.Heshima kamili huwepo hata kama haupo pale anapokuwa na wengine kwa hiyo kuwa makini na kile mpenzi wako anachokisema nyuma yako wakati wewe unapokuwa haupo utagundua tu.

3.Haulizi ushauri wako:Kuuliza ushauri wako ni tofauti na kuomba ruhusa,kuomba ushauri kutoka kwako ina maana kuwa anathamini sana mawazo yako na hakiri yako pia.Kuomba ruhusa ina maana hapendi matatizo lazima utambue utofauti pale unapotaka kujua kuwa anakuheshimu au la.Lazima asikilize kwa makini unapokuwa unaongea kuhusu swala flani ulilomuuliza.Sio tu lazima asubiri ndiyo au hapana kutoka kwako,anakuheshimu sana kiasi ambacho anataka asikie unamawazo gani yatakayomfanya asonge mbele zaidi.

4.Haheshimu vitu unavyovijali:Mwanamke anaye fake heshima anaweza akajifanya anakuheshimu wewe lakini utagundua kuwa haheshimu vitu vya msingi sana unavyovijali wewe.Huwa hana raha anapokuwa karibu na familia yako,rafiki zako,au hata rafiki zako ambao wana maana kubwa sana kwako kuwa makini kumgundua.

5.Anazungumzia wanaume wengine:Je Msichana wako anapenda kuwazungumzia wanaume wengine wanao mvutia??Au huwa anapenda sana kukaa au kuzungumza na rafiki zako au wanaume wa rafiki zake??Hii ni njia ya kipekee sana ya kukuonyesha kuwa huna mvuto tena kwake,anaweza asikwambie,lakini kusumhua hakili yako kwa kuzungumzia wanaume wengine ambao wanamvutia ni alama mbaya sana ya utovu wa heshima kwako.