Wednesday, April 11, 2018

Dalili Kumi za Mwanaume Ambaye Hana Pesa, Mwanamke Jiongeze..


1. Kila siku appointment zake yeye ni gheto kwake au anang'ang'ania kuja kwako, hakuna hata kwenda beach wala hotelini.

2. Siku ukiwa unaenda kwake, anakwambia njoo kwenye saa tisa au kumi. Ujue amekadiria hiyo mida utakuwa umeshapata lunch.

3. Ukiwa unaenda kwake hasemi ukikaribia nishtue nitoke kukupokea, ujue anaogopa akifika kabla yako itabidi alipie bajaji.

4. Ukiwa unaondoka kwake anasema sijisikii vizuri kwahiyo siwezi kukusindikiza, ujue anaogopa unapopanda bajaji itabidi akulipie.

5. Ukimwambia umefulia, anakwambia "pole mpenzi ndiyo maisha hayo" ujue hana cha kukupa.
6. Mkiwa mpo mahali inabidi kila mtu aondoke peke yake ukasikia anasema mimi nitapanda bajaji pale mbele kuna sehemu napitia, ujue hana hela anaenda kupanda daladala.

7. Kila mkienda kula restaurant jamaa anasema "mimi nimetoka kula sio muda njaa haiumi" haagizi hata maji ya kunywa ujue jamaa hana kitu.
8. Kama upo mtandao tofauti na yeye kila siku yeye anatuma tu sms, siku akitaka kupiga simu anakwambia "weka line ya tigo tuongee" ujue hana kitu huyo.
9. Ukiona anasisitiza kwamba hapendi wanawake wanaopenda vitu vya gharama kama simu n.k, ujue kaishiwa huyo akaoe ma house girl.

10. Ukiona kila siku ukikaa nae anakupa wosia kwamba mapenzi sio pesa, ujue hana kitu huyo.