Saturday, November 18, 2017

MAHITAJI YA MWANAMKE: JITAHIDI KUMFANYA MPENZI WAKO AFURAHI


a+woman+deep+thinking[1]

MAHITAJI YA MWANAMKE

1.     Mvuto na ukaribu (affection) – maneno na matendo yachochee mvuto na ukaribu, Kwamfano. Kukubali alivyopendeza, kumsifia nk

2.     Mazungumzo (conversation) – mwanamke huumizwa sana na vipindi virefu vya ukimya, sio tu kwamba wanataka mazungumzo bali mazungumzo yenye hamasa na mvuto


3.      Kumwamini (trust) – mwanamke anakiu ya kuaminiwa, anataka mtu aliye muwazi, asiye ficha kitu chochote, anatamani umwamini na sio kuhofia kila anachokifanya au kumhofu kila aliyeko naye

4.     Ulinzi (security) – mwanamke anapenda kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake kiafya, kihisia, na kiuchumi. Sio yeye tu bali na familia yake yote.


5.     Ushirikishwaji ktk mambo ya familia (participation) – Sio kila kitu kinafanyika yeye hajuo, anaona tu vitu vinaenda kama vile yeye sio mmoja wa wanafamilia na mzazi. Mfano, anagundua unasomesha ndugu yako pasipo hata yeye kujua. Mwanamke anatamani kuona anashirikishwa katika yote yahusuyo nyumbani kwake maana kwake nyumbani ndiyo kitovu cha maisha yake zaidi ya kazi yake na marafiki zake..........