Thursday, April 26, 2018

UFAHAMU UGONJWA WA U.T.I NA MATIBABU YAKE..[URINARY TRACT INFECTIONS]

ugonjwa wa uti ni nini?
huu ni ugonjwa ambao unashambulia njia ya mfumo wa mkojo, ni kifupi cha neno urinary tract infections..ugonjwa huu unashambulia 1% mpaka asilimia 3% ya ya watoto wa shule ya msingi lakini unazidi kuwashambulia zaidi wanavyozidi kukua kiumri kutokana na kushiriki sana tendo la ndoa.
ugonjwa huu hushambulia sana wanawake wenye miaka 20 mpaka 50 na mara chache sana mwanaume wa chini ya miaka 50 anaweza kushambuliwa na ugonjwa huu.kumbuka ugonjwa huu haumbukizwi kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke ila ngono huchangia bacteria kushambulia njia ya mkojo ya mwanamke. hivyo ukiugua wewe haimaanishi na mwenzako atibiwe labda kama imegundulika kuna ugonjwa wa zinaa umeambatana.

                         mambo yanayochangia mtu kuugua ugonjwa huu.
jinsia; wasichana wanaugua sana ugonjwa huu kwa sababu ya ufupi wa mrija wao wa kutoa mkojo{urethra], mrija huu ni mrefu sana kwa wanaume kiasi kwamba sio rahisi kwa bacteria kusafiri na kufika wa mrija na kushambulia.
lakini pia umbali mfupi kati ya uke na mkundu kwa wanawake, hii inaweza kusababisha bacteria kuhama kirahisi kutoka kwenye mkundu na kushambulia njia ya mkojo hasa kwa wanawake wanaochamba na maji kutoka nyuma kwenda mbele.
magonjwa ya zinaa na magonjwa ya tezi dume pia huweza kuchangia kuugua kwa ugonjwa huu kwa wanaume.

ujauzito; asilimia 2 mpaka 8 ya wanawake wajawazito huugua ugonjwa wa u.t.i kwa sababu ya kutanuka kwa mrija wa mkojo na kusabisha kutuama kwa mkojo ndani ya mirija hiyo.

kuziba kwa njia ya mkojo; kuziba kwa aina yeyote ya njia ya mkojo huweza kusababisha ugonjwa huu. mara nyingi husababishwa na magionjwa ya zinaa.

magonjwa ya mishipa ya fahamu; magonjwa yeyote yanayoathiri mishipa ya fahamu na na kusababishwa mkojo kushindwa kutoka kawaida husababisha ugonjwa wa u.t.i

bacteria; hawa kitaalamu wanaitwa e.coli, asilimia 80% ya wagonjwa u.t.i hushambuliwa na bacteri a huyu.

kurithi; kuna ushahidi kua ugonjwa huu unaweza kuathiri familia fulani fulani kutokana na matatizo yao binafsi ya kimaumbile.

kushuka kwa kinga ya mwili sababu ya magonjwa au chakula kibovu.

                                        dalili za ugonjwa ya u.t.i
ugonjwa huu una dalili mbalimbali kutokana na viungo ambavyo vimeathirika kama ni kibofu cha mkojo, figo, au mirija ya mkojo kama ifuatavyo..
  • maumivu wakati wa kukojoa..
  • homa 
  • kuumwa tumbo
  • kutapika na kuharisha
  • kukojoa mara kwa mara na hisia za kutaka kujikojolea ukichelewa chooni.
  • maumivu ya misuli 
  • kujikojolea kitandani hasa kwa watoto
                                                   vipimo vya u.t.i
  • urinalysis; hichi ni kipimo kinachopatikana hospitali nyingi nchini, hutumia kitu kama njiti kitaalamu kwa hiyo kazi[dip stick]. kuonekana kwa damu au seli nyeupe za damu kwenye mkojo ni kiashiria cha ugonjwa huu.
  •   urine for sediments; hii ni njia ya kutumia kiasi kidogo cha mkojo na kupima kwenye darubini kuangalia damu na seli za usaha ambazo ndio uhakiki wa u.t.i
  • kipimo cha utrasound scan; wakati mwingine kama mgonjwa ana dalili za kushambuliwa kwa figo kipimo hiki hutumika kuangalia ni kwa kiasi gani figo zimeharibika.
                                                               
                                                         matibabu
matibabu ya uti hutegemea hali ya mgonjwa na majibu yatakavyoonyesha, kama hali ni ya kawaida mgonjwa hupewa vidonge na kama hali ni mbaya sana mgonjwa huchomwa sindano.
vidonge hivyo ni kama cotrimoxazole, ciprofloxacin, lomefloxacin, na kadhalika na sindano ni kama gentamycin, cefriaxon na ampicilin..
dozi ya mgonjwa hutegemea umri na uzito wake lakini pia kwa mama wajawazito usimeze dawa yeyote ambayo hujapewa na daktari kwani baadhi ya dawa tajwa hapo juu sio nzuri kwa mama. dawa salama kwa mama mjamzito mwenye uti ni amoxycillin, ampicilin na cefriaxon.
mara nyingi wanaume huchanganya kati ya uti na kisonono, kwa kawaida kama mwanaume una uti hakuna uchafu mweupe unaotoka sehemu za siri lakini pia kama mwanaume ana uti dawa ya kumeza ya kuanzia ni doxycline kimoja kutwa mara mbili kwa muda wa siku saba na kama mtu ana tatizo la tezi dume yaani prostitis dozi hii hongezeka mpaka siku 14 mpaka 21.
kumbuka kunywa maji mengi sana wakati unaumwa hii husaidia kusafisha figo na kupona haraka.
                                              jinsi ya kuzuia ugonjwa huu..
  •  hakikisha choo unachotumia ni kisafi, kwa wanawake mwaga maji kabla ya kukojoa kisha mwaga maji baada ya kukojoa mara nyingi ile kuchuchumaa kukojoa mkojo hugusa choo kwa presha kubwa  na kukurudia kwenye sehemu za siri.
  • baada ya kujisaidia choo kubwa chamba kutokea mbele kurudi nyuma ili usihamishe bacteria wa mkunduni kwenda kwenye uke.
  • tumia dawa ya kuzuia uti kwa watu ambao inawapata mara kwa mara. mfano kama umegundua kila ukishiriki ngono unaugua basi meza dawa za kuzuia ugonjwa kuanza kila baada ya kushiriki kwa siku kwa dozi ya siku moja tu kwa dawa nilizotaja hapo juu.. mfano cotrimoxazole vidonge viwili tu kwa siku. wajawazito na wanaume wanapata sana ugonjwa huu mfululizo nao wanashauriwa kutumia dawa pia. wajawazito watumie amoxyline au ampicilin mbili kila siku. wanaume watumie doxycline mbili kwa siku.
  • kakojoe haraka unapobanwa na mkojo na hakikisha umekojoa mkojo wote
  • kakojoe mara tu baada ya kushiriki tendo la ndoa.
  • usitumia sabuni zenye kemikali sana kusafisha sehemu zako za siri.
  • usivae nguo zianazobana sana au chupi za kutengenezwa na nailon, tumia chupi za pamba.
mwisho; ni ngumu sana kwa mwanaume kuugua uti na ukimuona anaumwa ni vizuri kuhakukisha kweli kama sio ugonjwa wa zinaa kwa kuminya uume na kuangalia kama kuna uchafu mweupe unatoka. kama uchafu upo hiyo sio uti bali ugonjwa wa zinaa. ugonjwa huu ukipuuziwa muda mrefu huwea kuua figo kabisa.