Friday, November 17, 2017

JINSI/NAMNA/MBINU ZA KUIMARISHA MAHUSIANO

Jose Mourinho ni binadamu mwenye akili ya aina yake. Na kila anapotembea anawaza uhuni tu, ajawahi kunivutia katika namna ya soka ambalo amekuwa akifundisha, lakini historia yake, haidanganyi. Historia yake inanisuta, na inanifanya nitafakari kwa muda. 

         Ameishi kwa kuamini kile anachoamini na kila mitaa anayozunguka katika nchi mbali mbali za ulaya hakuondoka mikono mitupu, hii ni kutokana na mbinu zake za kibunifu katika mchezo wa soka dhidi ya wapinzani wake.
Hiyo imenifanya nijifunze kitu ndani yake ilinami niweze kufanikiwa kwenye mchezo wa mapenzi na mahusiano ambao umekuwa ukinitoa chozi kila kukicha. Baada ya kufanya utafiti wangu kwa muda takribani ya mwaka na nusu nimefanikiwa kuzikamata mbinu ambazo mpenzi msomaji kama utafanikiwa kuzipata. Hakika nawe utanifikiwa kwenye maswala ya mahusino na mapenzi, kama ulivyo kwa Jos’e Mourinho kwenye   Mchezo wa soka.
Kwanza kabisa, jifunze kucheka naye pamoja: Kicheko Ni mlango wa ukaribu, kama mnaweza kucheka pamoja basi mnaweza kulia Pamoja. Kicheko kinaongeza faraja kwenye mapenzi. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali Katika Kila Kitu. Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea Kwenye Kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa Kutolea kile kilichokukwaza. Kama utaweza kuwa katika namna hii basi, ni rahisi kutatua matatizo yenu yanayowasibu wote kwa pamoja bila kuwa na hofu miongoni mwenu. Kwa namna hiyo inasogeza ukaribu kwenye mahusiano, na daima inachagiza kuimarisha mahusiano yenu.
               Jifunzeni kumtia moyo mwenza wako:  jaribu kuwa msada mkubwa kwa mwenza wako wa hali na mali kadri uwezo wako unavyokuruhusu. Katika namna nyingine, ongeza usikivu kwa mwenzako. Onyesha heshima kwake, pia kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokuwa naye  peke yake. Mjenge mwenzako mbele ya  wengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee Yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila Afanyalo. Namna unavyoonesha unamjali na unamtia moyo, jambo hili linaongeza
nafasi kwenye penzi lenu.
             
          Jifunze kupenda kugusana kila wakati na mwenza wako: Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima ujifunze kujenga tabia ya Kugusana na mwenzio, mara upatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala. Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono, mkiongea au mkitembea, kukumbatia vile vile kuchezea nyewele za mwenza wako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili.  Mguso unaongeza ukaribu na furaha ndani ya miili yenu, kiasi cha kwamba uthamani wa kuhitajiana na kupendana unaongezeka kwa namna hii, inaongeza na kuimarisha mahusiano yako.
Zungumza na mwenzio hisia zako: Mawasiliano ni kitu kikubwa sana kwenye mahusiano, mawasiliano huendesha mapenzi, pasipo mawasiliano hakuna mapenzi. Kwa maana mawasiliano ndio yanachangia kwa kiasi kikubwa kuonesha ni jinsi gani umeguswa na mwenza wako. Hivyo jaribu kwa kiasi kikubwa kuzungumza na mwenzio kwa namna gani unajisikia dhidi yake. Jiwekee muda wa kutosha wa kuzungumza na mwenza wako, ilikufahamu yale yanayomsibu na hata kuweka mipango kwenye maisha yenu. Mikakati ni muhimu penzi lisilo kuwa na mikakati halichelewi kuyumbishwa. Zungumza naye ujue anawaza nini kuhusu wewe. Mpe nafasi ya kuzungumza. Ukiweza kuhakikisha jambo hili hakika mahusiano yako, yataendelea kuwa imara muda wote.
        Jifunze kusamehe: Kamwe usiache maumivu na machungu yatawale uhusiano wako. Lazima ujifunze kumsamehe umpendao. Safari ya mapezi kutwa haiachi kuwa na misukosuko, hivyo mwenzako akionesha amekiri kosa, kunjua moyo wako na humuoeshe ni kweli moyo wako upo wazi kwa lile unenalo juu ya kumsamehe mwenzako. Hii itawahamarisha sana.
Hitimisho: Penzi linahitaji mbinu za kibinifu, jifunze wakati wote kumsoma mpenzi wako, katika maana halisi, mdekeze, huku ukimsifia kwa anye asijutie kuwa na wewe kwenye maisha yako. Mfanye amini zaidi kuwa wewe ni chaguo sahihi kabisa na hakukosea katika maamuzi yake. Ongeza ukaribu zaidi huku ukiongeza usanifu na utimilifu wa akiri katika kuyaongoza mahusiano yenu katika namna kama hii itakufanya mwanzako ajisikie raha kuwa nawe.