Wednesday, November 29, 2017

Je Kupigana Denda au Mate unaweza pata HIV? Jibu hili hapa kumbe ni balaah

Hi! Admin, watu wengi wamekuwa wakifanya "romance" kupandisha mihemko ya kufanya mapenzi kwa kunyonyana ndimi,baada ya hapo wakiwa kwenye sita kwa sita mwanaume anavaa condom je atakuwa salama hapo nakama atakuwa si salama atumie njia gani awe salama?

Na unyonyaji wa viungo vya uzazi M'O na K vinachangia maambukizo kwa sababu nafikiri asilimia 95 ya wanawake wa BONGO hupenda sana kufanyiwa hivyo. admin ubarikiwe sana kwa elimu unayotoa.Wako Djunior.

Jawabu: Hakika unaweza kupata vijidudu vinavyosababisha Upungufu wa Kinga Mwilini(UKIMWI) kwa kula denda na kwenda chumvini. Japokuwa watu wengi wanakuwa "relax" na denda kwa vile wanajua kuwa mate hayabebi vijidudu lakini ukweli ni kuwa kilichomo kinywani sio mate tu bali kuna taya za ju na chni, kuna mashavu kwa ndani, kuna sehemu chini ya ulimi, ukienda kwa ndani yakinywa kuelekea kwenye koo pia kuna vijikona kona.


Sehemu zote hizo nilizozitaja zinaweza kupata mchubuko/mpasuko kirahisi kutokana na sababu tofauti ikiwa ni pamoja na kula vitu vitamu lakini vikali kama vile nanasi, matunda ambayo yana choma-choma miwa na embe ng'ong'o vinahusiaha nakadhalika.

Kwa bahati mbaya sio rahisi kwako wewe kujua kama unamichubuko sehemu za kinywa chao isipkuwa pale mchubuko unapobadilika na kuwa kijidonda na njia pekee ya kugundua ni wakatiunapokula kitu kichachu au cha moto sana au chenye chumvi nyingi.

Sasa ikiwa wewe na mhusika unaembusu mnamichubuko hiyo ndani ya vinywa vyenu hapo ndio uwezekano mkubwa wa kubadilishana damu iliyo na vijidudu iliyojichanganya kwenye mate unapotokea namatokeo yake ndio Ngoma.

Suala la kumshukia ndio hatari zaidi kwani ule ute wa mwanamke na ule wa mwanaume (sio Shahawa bali ule ute wa mwanzo) unabeba vijidudu na hivyo unaweza kupata vijidudu kama kinywa/koo lako lina michubuko.

Nakushauri ufanye hivyo na mtu ambae ni msafi kiafya (mkapime), vinginevyo tumia kinga (Condom) na hakikisha unaepuka kubusuMate na kulamba-lamba huko kunako, kwani kama wewe bado ni "hit & run" basi hakikisha una-focus kwenye ngon tu.

Nikisema ngono tu, nina maana kuunganisha uume na uke kwa kutumia Condom na hatua nyingine za kimahaba achana nazo na uzifanye na mpenzi wako ambe ni wa uhakika, unampenada na mnahaminiana.

Asante kwa ushirikiano.