Monday, October 1, 2018

SHEMEJI HIYO MITEGO YAKO DAWA YAKO IKO JIKONI WE HAYA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsz-RWlu1PPHx6xwUXqTZ6B2nIKIdbnkwVSfnm4kuwZguSjkeaW8rpPNITbwQ1ujeOwdJOf5jyqyV_-GeSFzX8oYe-NiIs5lGmULVdKkcvHnpEcHpeJIn87FPJAVwFVTwIuHlbfPUoJqs/s640/umejuaje.jpg
 Katika maisha yangu napenda sana amani ndio maana huwa najisikia vibaya sana ikitokea nimemkwaza mtu wangu yoyote wa karibu kwani najiuliza atanisamehe kweli kwa hili kosa nililomfanyia?
Historia ya maisha yangu imenifanya niwe na moyo huu wakutopenda kumkwaza mtu kwani nimefadhiliwa sana na kaka yangu,nimepewa kila kitu muhimu ambacho kijana anastahili awe nacho kama vile simu nzuri,pesa ya matumizi achilia mbali ada ya masomo ya shule za private nilizosoma kuanzia kindergarten mpaka nimefika chuo kikuu,Kwa kweli kaka yangu ni mtu wa pekee sana maishani mwangu na hakika siwezi kulipa fadhila zake. 
Ameniamini sana kiasi cha kuwaananiachia gari lake anaposafiri niwehuru kulitumia muda wowote nitakao lakini kwa bahati mbaya moyoni nimekuwa mwenye huzuni sana kwani mke wa kaka yangu yaani shemeji amekuwa tatizo kila kaka akisafiri maana vituko anavyonifanyia sio siri nahisi kutamani kuhama kwake pasipohata kujua nitaenda wapi. 


Shemeji anathubutuje kunitolea chozi akinililia eti anataka niwe namimi kimapenzi wakati unajua fika kwamba hili si jambo linalokubalika hata kidogo,hakika shemeji uzuri wake anautumia kama chambo cha kutaka kuninasia, zaidi ni pale anapokuwa ananavaa vinguo ambavyo ni robotatu uchi tena unategea tukiwa wawili tu nyumbani.
Hakika siwezi kulipa ubaya kwa wema kwani kaka yangu ndiye tegemeo langu na furaha yangu,yeye wala hajali hilo labda kwakuwa anajua fika kwamba kaka anampenda sana na hawezi kuamini neno lolote aambiwalo kuhusu yeye,kwanini lakini wataka kuharibu  undugu wetu mimi na kaka yangu? 

Shemeji afanye lingine lolote ila suala la kutaka nifanye ngono na yeye  kwani atafanya kwa mara ya kwanza nione gadhabu ya kaka yangu ambayo sikuwahi kutegemea kuona juu yangu,shemeji ananikosesha raha ya maisha kwani amekuwa king’ang’anizi isivyokawaida mpaka baadhi ya majirani wameanza kuhisi kitu. Amefikia pabaya sasa shemeji that’s not fair at all please give me a break.


 Tafadhali unaushauri gani kwa huyu kijana aliyeandika waraka huu ambaye kwa kweli anatatizo  hili sugu ana shindwa afanye nini?Toa ushauri wako uwe msaada kwake.