Thursday, April 12, 2018

Njia 10 za Kutongoza Kwa Macho Ambazo Hufanya Kazi

 
Je wataka kujifunza jinsi ya kutumia macho yako kupitisha ujumbe wa kuonyesha umevutiwa na mtu fulani?

Kutumia macho kama mbinu ya kutongoza ni njia rahisi ya kupitisha ujumbe kutoka kwako hadi kwa yule unayemzimia kwa urahisi bila hata kutamka neno lolote.
Mwanzo mchezo wa kutumia macho kama mbinu ya kutongoza huwa ina raha yake kiasi flani.

Uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa ni rahisi kufahamu kiwango gani mtu amevutiwa nawe bila kuwauliza kuwatoa out. Pili ni kuwa uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa unamjulisha unayemzimia na mapema ya kuwa umewavutia hivyo kujitayarisha na mapema iwapo atakubali kufanya maongezi na wewe.

So ni mbinu zipi hizo unazoweza kutumia kumvutia unayempenda bila kuonekana kama fala?

Njia za kutongoza kwa kutumia macho

Utafanya nini iwapo umemuona yule aliyekupendeza katika mkahawa ama katika party ulioalikwa na marafiki zako? Kama hujui la kufanya basi tumia macho yako kumtongoza ili kumfanya avutiwe nawe kiurahisi.
Fanya kutumia mbinu hizi 10 tulizoziorodhesha kupitisha ujumbe wako mara moja.
1. Mwangalie mara kwa mara kikawaida
Umemuona yule aliyekupendeza? Fanya kumuangalia mara kwa mara kikawaida. Itafikia mahali flani pia yeye atanotice ya kuwa umekuwa ukimuangalia kwa muda hivyo utaiteka atenshen yake.
2. Badilisha kwa kuangalia 'kimukhtasari'
Usiwe na pupa ama utaonekana kama stoka. Hivyo yule unayemzimia akikuona unamuangalia halafu aanze kukuangalia kiudadisi, wewe mwangalie kwa sekunde moja halafu ghafla angalia kando.
3. Rudia kumuangalia
Mtizame tena unayemzimia. Mwangalie, lakini angalia kando mara moja wakati ambapo atakuangalia. Usizubae, mwangalie tena kwa sekunde nyingine moja kwa mara nyingine. 
4. Mfanye ajue kuwa yuko akilini mwako
Mara ya kwanza, unayemzimia ataona ya kuwa kumuangalia yeye ilikuwa tu ni kupita njia. Lakini wakikushika mara kwa mara unawaangalia wataanza kuingiwa na hisia ya kuwa wewe umevutiwa nao. Usimwangalie zaidi ya sekunde moja ama utaua msisimko ambao unaanza kujenga kati yenu.
5. Jenga msisimko
Ok kufikia sasa itakuwa umeteka atenshen ya yule umemzimia na mara kwa mara atakuwa akikuangalia kuchunguza iwapo unamuangalia au la, sasa kilichobaki nikujenga msisimko. Jizuie kumwangalia kwa madakika. 
Kufanya hivi kutamfanya yule unayemwangalia kutaka kujua kwa nini umeacha kumuangalia hivyo atakuwa mara kwa mara akikuangalia ili kuhakikisha ya kuwa unamuangalia au la. Mbinu hii inamfanya pia yeye kuingiwa na msisimko wa kuendelea katika huu mchezo. 
6. Fanya mjeuko
Umemnotice yule unayemzimia yuko pembeni mwa jicho lako. Mwangalie bila kujeuza kichwa chako. Ngojea mpaka ule wakati atakapokuangalia. Ukimwona anakuangalia, fasta jeuka uanze kumuangalia. Kufanya hivi kutakuwa kunaleta dhana ya kuwa ni yeye ndiye anayekuangalia na wala si wewe. Pia inaleta dhana ya kuwa wao ndio wamevutiwa na wewe na wala si kivingine.
7. Mwangalie kwa muda mrefu
Kufikia sasa mumekuwa mkibadilishana macho kimukhtasari na yule unayemzimia. Sahizi atakuwa anakungojea umuangalie kwa mara nyingine. Well, wakati huu wakati ambapo utamwangalia, mwangalie zaidi ya sekunde moja halafu angalia kando.
8. Tabasamu na tahayari
Ongea na marafiki zako ama jikeep buzy, halafu mwangile sekunde moja au mbili. Na kila mara utakapomwangalia tabasamu ama tahayari kikawaida. Usitabasamu kama unamwangalia. Ngojea mwanzo mpaka uangalie kando halafu ndipo utabasamu.

9. Angalia mwitikio wake
Ok je huyu unayemuangalia pia yeye anakuangalia mara kwa mara? Kama jibu ni ndio, basi mbinu hii inafanya kazi na inaonyesha dalili ya kuwa siku yako itakuwa ya furaha na haitapotea hivi hivi. Iwapo itatokea huyu unamwangilia haonyeshi dalili zozote za majibu, ni dhahiri ya kuwa hujawavutia hivyo ni vyema ujiondoe ama ujipatie shughli mbadala. Hauwezi kushinda wakati wote katika mchezo wa kutongoza kwa macho.
10. Tabasamu unapomwangalia
Kufikia sasa unauhakika ya kuwa huyu unayemwangalia mara kwa mara anaonyesha dalili ya kupendezwa nawe. Hatua utakayoichukua sahizi hakuna cha kurudi nyuma. Katika moja wapo ya kumwangalia, mwangalie direct kwa macho yake halafu vuta tabasamu refu. Kama pia atajibu kwa kutabasamu, utakuwa umeufunga mchezo. Iwapo unayemwangalia atakuangalia na mshangao basi anahitaji muda kiasi kabla kufanya approach ya mwisho.

Kama huu mchezo umefaulu kwako, hivi ndivyo unavyopaswa kufanya. Kama wewe ni mwanamke mpatie nafasi ya huyo mwanaume aongee na wewe. Na kama wewe ni huyo mwanaume wangojea nini? Chukua hatua ya haraka!