Wednesday, October 3, 2018

Jinsi ya kumpagawisha mpenzi wako, kumteka moyo na akajikuta anakupenda Zaidi na Zaidi.



Kiumeni.com tunachokuambia sio sura yako au swaga zako ndo zitakazo mfanya msichana akupende Zaidi ya yeye atakavyo, ila ni kwa jinsi wewe unavyomfanya ajisikie akiwa nawe, jinsi anavyojihisi na kupokea upendo unaotoka moyoni kwake na kuukubali, ndicho kitu kikuu kitakacho mfanya mpenzi wako apagawe nawe na kujikuta akikupenda kupitiliza.


Hakikisha kila mda unaotumia nae unamtengenezea kumbukumbu nzuri, afurahie vitendo mnavyofanya pamoja na kutengeneza historia yenu wawili, kumbukumbu zinazomburudisha moyo wake kiasi hata ukiwa mbali na akazifikilia, zinamfanya atabasamu na hisia za kukumisi kumjaa mara dufu, hizo hisia za kumtaka awe tena karibu yako zimfanye asiache kukutafuta kwenye simu na kukutumia meseji.


Mfanye ajione tofauti, ajihisi unamwona spesho na sio kwa sifa unazompa ila kwa jinsi unavyomchukulia, aone kwa vitendo, aamini kwa macho yake mwenyewe, hii itamfanya akupende bila kujihisi, afanye vitu kwa jinsi mapenzi yanavyompeleka yeyewe, ajitoe kwa moyo na kukuona kuwa nawe ni bahati hivyo atajikuta anaitumia hio bahati kwa marefu na mapana, huku akiwa ajiulizi wala kujishuku.