Wednesday, November 21, 2018

Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani. 1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo: Wanawake ambao hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu. 2. Huongeza ukakamavu wa mifupa: Wanawake waliokoma kupata hedhi (menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis. 3.Hupunguza msongo wa mawazo: Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, muscle relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema. 4. Hupunguza maumivu: Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom). 5. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume: Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi. 6. Huongeza uwezo wa kunusa: Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo (brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu (brain olfactory bulb). 7. Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema: Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi. 8. Huongeza kinga ya mwili: Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali. 9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke: Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa. 10. Hudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida: Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa. 11. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini: Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini. 12. Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke (vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection ). 13. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini: Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini. 14. Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako: Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote. 15. Husaidia kuishi kwa muda mrefu: Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele. DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako. 16. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa. 17. Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba: Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne.

Wanasanyans wamesema ya kwamba manii(semen) yanayotolewa na mwanamume wakati wa kujamiana na mwanamke yanasaidia mwanamke kuwa na uwezo wa kushika mimba.Kulingana na utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa kimataifa chini ya Gregg Adams na kuchapishwa katika jarida la proceedings of the National Academy of Sciences, umesema ya kwamba manii sio tu hubeba shahawa (sperm) za mwanamume kwenda kwa mwanamke bali pia huchochea mayai ya mwanamke (ovaries) kutoa mayai ya uzazi.Protini inayopatikana katika shahawa inayojulikana kama Ovulation-Inducing Factor au IFO, ndio hasa huchochea sehemu ya ubongo inayojulikana kama hypothalamus kwenye ubongo wa mwanamke kutoa homoni ambazo hupelekwa moja kwa moja kwenye mfumo wa neva na kisha homoni hizo hupelekwa kwenye mfumo mwingine wa homoni unaojulikana kama endocrine system.

Homoni hufika kwenye mfumo huu wa endocrine system kupitia sehemu ya ubongo inayojulikana kama pitituary gland na hivyo kuingia kwenye mzunguko wa damu.Baada ya kufika wenye mzunguko wa damu, homoni hizi huenda moja kwa moja mpaka kwenye mayai ya mwanamke (ovary) na kuyachochea mayai haya kutoa mayai ya uzazi(ovum) katika hatua inayojulikana kama ovulation.

Watafiti hao wamesema wamegundua protini hii aina ya IFO katika shahawa za wanyama aina ya ilamas, sungura na hata kwa binadamu. Wanyama wengi wana viungo vya ziada vya kujamiana ambavyo hutoa manii kwenda kwenye shahawa lakini umuhimu wa manii hayo bado haujagundulika.


“Wazo la kuwa kuna chembechembe katika manii ya wanyama na binadamu ambayo huchochea ubongo wa mwanamke ni wazo geni kabisa, alisema Gregg Adams”.
Wanasayansi hao wameweza kugundua ya kwamba ni chembechembe hizi ndizo pia husaidia katika ukuaji, urekebishaji na ustawishaji wa seli za neva.


Katika utafiti huu ambao wanasayansi walitumia ngombe, ilamas na binadamu, wanasayansi hao waliweza kugundua protini aina ya Ovulation-Induced-Factor kutoka katika manii ya wanyama hawa pamoja na binadamu waliohusika katika utafiti huu.
Wanasayansi hao waliwachoma sindano yenye protini hii wanyama aina ya ilamas na kuwafanya wanyama hao kupata ovulation wakati walipowachoma ngombe sindano yenye protini hii aina ya IFO, ngombe hao walishindwa kuingia katika ovulation lakini protini hiyo iliweza kuwafanya ngombe kutengeza mifuko kwenye mayai yao ambayo ndio hasa hubeba mayai ya uzazi na hivyo kuwafanya ngome kuwa tayari kwa kushika mimba.Pia ilionekana ya kwamba protini hii (IFO) ina uwezo wa kustawisha mimba kwa ngombe hawa.
“Utafiti huu mpya unaongeza uelewa wetu wa mfumo wa ovulation lakini pia huongeza maswali mengi juu ya ovulation hiyo’, alisema Adams”


Tafiti zaidi zinahitajika ili kujua ni kazi gani ambayo protini hii aina ya IFO hufanya katika kumpa mtu uwezo wa kutunga au kushika mimba.Wanasayansi hao wanahisi uwepo wa protini hii kwa wingi kwa baadhi ya wanaume inawezekana ikawa ndio chanzo cha kuwafanya wanaume hao kuwa na uwezo mkubwa wa kutungisha mimba mwanamke (fertile).


Ovulation ni hatua ambayo yai la uzazi hutolewa na kwenda katika mfuko wa uzazi (uterus) na kusubiri shahawa ili lirutubishwe na kuwa mimba.Ovulation hii hutokea siku ya 14 baada ya mwanamke ya kuanza hedhi yake.Yai la uzazi ambalo hutolewa wakati huu hukaa kwa masaa 48 kusubiri kurutubishwa na kama halitarutubishwa na shahawa basi yai hili huharibika na kutolewa nje kama hedhi.

Ni katika ovulation, ndio mwanamke huwa na uwezo/asilimia kubwa ya kushika ujauzito kama atajamiana na mwanamume.Dalili za ovulation ni pamoja na kichwa kuuma, kizunguzungu, kichefuchefu, matiti kuuma, kuongezeka kwa kiwango cha joto mwilini, kutokwa jasho kwa wingi usiku, kubadilika ladha ya ulimi, kuwa na hasira mara kwa mara, kupata hamu ya kujamiana, kutokwa na ute katika tupu ya mwanamke ,maumivu ya tumbo, maumivu ya mgongo