Wednesday, October 3, 2018
Jinsi ya Kuanzisha Ngono
...kwa mwanamke
Mimi nilikuwa napenda kuwauliza akina dada(wanawake kwa ujumla), mfano mume wako(hasa wale walioko kwenye ndoa) kaja kukutaka, na wewe hujisikii, kwa sababu zisizo za lazima.
Na mume wako ndio mambo yamekuwa mambo, na wewe mwenyewe unaona, utafanyaje ili muridhishane?Nazungumza hivi nikiwa na maana kuwa kuna ndoa nyingi zimeingia mtegoni/matatani kwa sababu ya hili, kwamba mwanaume au mwanamke hapati tendo hilo kila anapohitaji.
Tukirejea kwenye mistari tunaambiwa mke au mume ni mashamba yenu....msinyimane nk, sasa je hali hiyo ndio hivyo mnanyimana iweje?Nilisikia mwanamke mmoja akilalamika kuwa mume wake siku hizi akirudi nyumbani anaangalia ukutani/ anampa mkewe mgongo, sababu hasa haijui!
Anahitaji tendo, anahamu ya mapenzi na mumewe lakini mumewe anarudi hoi, sababu ya kazi ngumu, au ndio hajisikii, au ndio sijui kwanini(Na wanawake wengi hata wale waliopo kwenye ndoa hawajui kumtamkia mumewe kuwa ninahitaji tendo...au sio)!
Hali kadhalika wapo wanawake wengi wa namna hiyo, ambao hawapendi mara nyingi kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, na wakifanya wanafanya kama wamelazimishwa!`kila siku kila siku...aaah, mimi nimechoka...'
Sasa je hii inasababishwa na nini hasa? Hatuoni hii ndio inayochangia nyumba ndogo, na matokeo yake ni kuleteana magonjwa!Nimelielekeza hili swali kwa wanawake, je mume wako akikufanyia hivyo utafanyaje ili atimize wajibu wake?
Ndio hata kwa wanaume linawahusu, je na wanaume watafanyaje ili mwanamke atimize wajibu wake. Najua kwa wanaume wengi wanatafuta njia ya mkato-nyumba ndogo!Lakini nafikiri ipo njia njema na kama wengi tungekuwa tunafuatilia mafunzo tunayopata hapa tungefurahia mapenzi, lakini sidhani wote wanapita kwenye hii blog!
Soma tena