Monday, September 24, 2018

WANAUME TUWE MAKINI NA HILI


Kuna tabia fulani hivi mnawaalika Mademu Gheto wanakuja wanalala halafu ikifika asubuhi wanajua kabisa utaenda kazini,wao wanajifanya wamelala.

Utawas ikia 'Bebiii we nenda tu mi niache bado nna usingizi niachiefunguo utazikuta chini ya mlango' Kwa kumuamini unaacha..

DUNIA IMEBADILIKA... Mchawi sio lazima avae gagulo, mademu wa
siku hizi wanakupekecha hadi unakaa sawa, wanachukua nguo yako wanaipeleka kwa mtaalamu,wanaichezea Alingo na Azonto kwa Mpigo, ukirudi unakuta umepigiwa Pasi nguo za kwenda kazini kesho na gheto limepangwa,unajua yeesss..

Ukivaa tu ile nguo, na kwa vile Mungu kwako ni part time job kama Customer Care operator UNAKAMATWA... Usidhani Limbwata ni kwenye chakula au kuwekewa kipande cha Nyama kwenye kipapuchi, Watch out... Ni Sistaduu na ana sura ya upole lakini  
#NoTrust  ... wanaroga usitake Kujua, Ndoa zinasakwa kuliko Form 6 anavyopiga ruti ofisi za TCU..
Ukinitumia meseji ya mchango wakati wa harusi wiki6 zilizopita uliniambia utaoa maybe 2017 najua tayari umenaswa...

Ufunguo wa Gheto sikupi, amka tutoke wote, usingizi kwenu!