Saturday, September 29, 2018

MAZINGIRA YA CHUMBA YENYE KUAMSHA HISIA KALI ZA MAPENZI.

Mara nyingi tumekuwa tukiwaza mambo makubwa sana katika kuleta mvuto au mshawasha wa mapenzi hasa pale muwapo chumbani tayari kupeana tiba ambayo hakika humfanya kila mtu asahau shida. 

Hakuna haja ya kuumiza kichwa sana kwani yapo mambo mengi sana ya kuwafanya mpate hamasa wewe na mpenzi wako na mujione kuwa ni watu spesho kuliko wengine,moja ya jambo hilo ni aina ya taa iliyoko chumbani kwenu,taa hafifu na yenye rangi ya kuvutia kama vile rangi ya kijani,zambarau au pink ni silaha nzuri sana inayoamsha hisia za huba kwa wapendanao wawapo chumbani kwa sababu zifuatazo:-

*Taa za rangi na zenye mwanga hafifu huchangia kukufanya mpenzi wako awe na muonekano wa pekee wenye kuleta hisia zinazokuongezea matamanio kwani huonekana tofauti sana na awapo sehemu zinginekama vile awapo nje.
*Mwanga hafifu husaidia kupendezesha mavazi ya mpenzi wako kama vile night dress,briefs au knickers na kukufanya umuone kama malkia ambaye amekupa fursa ya pekee ya kuwa nae kwa usiku huo.

* Mwanga hafifu na wenye rangi ya kupendeza humfanya mwanamke/mwanaume wako kudeka na kutoa kauli zenye kuvutia zilizojaa maneno matamu kama vile ooh husband,swetlove,laaziz nk. hakika hayatakauka na hivyo kufanya shughuli yenu kuwa spesho na yenye upekee wa hali ya juu. 

Utafiti unaonesha kuwa kwenye mwanga mkali ni rahisi zaidi kumfanya mtu kujiamini kupita kiasi hivyo huweza kuchangia kutoa kauli zisizokuwa na dalili ya upole hivyo hupoteza raha kwa wale wakati huo maalum unapokuwa na mwandani wako.
Ni Jambo la msingi sana kuwa mbunifu katika mapenzi ili kuleta mahaba yatakayochangia kumteka mpenzi wako na kumfanya amiss uwepo wako pale anapothubutu kuwa mbali nawe hata kwa siku moja.