Tuesday, August 28, 2018

Maswali 40 Ya Kumuuliza Mwanamke Katika Deti

Ushawahi kutoka deti na mwanamke halafu ukafikia mahali katika chat yenu unaishiwa na maneno ya kuongea?

Ama umeagana na mwanamke mtoke deti siku ya pili halafu umekuwa ukikesha siku nzima ukiwaza ni maneno ama ni usemi gani utakaoongea siku ya pili wakati ambapo mtakutana?


Well, usiogope. Hapa umefika kwa zahanati ambayo itakutibu matatizo yako.

Hapa tumekuandalia maswali 40 ambayo utayatumia kumuuliza mwanamke na kuyafanya maongezi yenu yavutie na kumfanya mwanamke apendezeke na wewe hadi mwisho.

Well. Kabla ya kuorodhesha maswali haya kuna mambo ambayo unapaswa kufahamu:

  • Anza kwa kumsifia ama kumpendezea kwa mambo anayofanya mfano unaweza kumsifia vile alivyovalia, kazi yake, umbo lake nk.
  • Wakati utakapokuwa unamuuliza mwanamke haya maswali, hakikisha ya kuwa unatoa nafasi ya angalau sekunde 30 kabla ya kumuuliza swali la pili, yaani usimmiminie maswali yote wakati mmoja.
  • Hakikisha kuwa haulazimishi maswali yako, mwanamke akikataa kujibu swali lako jipe shughli kiasi kv unaweza kucheza na vidole vyako ama jambo jingine kabla kumuuliza swali lingine.
Baadhi ya mambo ambayo pia unapaswa kuzingatia katika rodha ya maswali haya ni kuwa:

Unapaswa kuyachanganya maswali yako. Maswali tuliyoyaorodesha hapa ni maswali yaliyowazi, yaani yanaweza kupanuliwa yakazua mada nyingine. Anza na maswali sahili kuangalia iwapo mwanamke unayezungumza naye anapenda kuongea au la. Pia muulize maswali yaliyo wazi ili kuongeza hoja yako.

Usimakinike na orodha ya haya maswali. Tumia maswali machache ambayo unayaona unaweza kuyatumia halafu ujeuza mada yako uanze kuongea maswala yako. Ukimakinika kutaka kutumia maswali haya yote basi unaweza kumfanya akuone hauvutii na anaweza kuboeka na wewe haraka sana.

Usihifadhi maswali haya. Hili ndilo jambo baya zaidi la kufanya. Ukikaa na deti wako huku ukirudia swali la kwanza hadi jingine unaweza kumfanya mwanamke aone kwamba unamfanyia mahojiano ya kazi. Unachohitajika ni kusoma baadhi ya maswali haya, yahifadhi kwa simu yako halafu yatumie wakati ambapo maongezi yako yanafifia.


Maswali yenyewe ni kama ya fuatayo...

1. Unaipenda hii sehemu?

2. Huwa unapenda kunywa kinywaji gani?

3. Mapochopocho unayoyapenda ni yapi?

4. Ushawahi kuja hii sehemu awali?

5. Siku yako ilikuwaje?

6. Unafanya kazi wapi?

7. Huwa unapenda nyimbo aina gani?

8. Unapenda salad aina gani?

9. Ni mkahawa gani unaoupenda zaidi?

10. Ni movie aina gani unapenda kuangalia zaidi?

11. Ni mambo gani unapenda kufanya baada ya kutoka kazini?

12. Unafanya mambo gani ili kujifurahisha?

13. Ulisomea wapi?

14. Sehemu gani unaipenda sana zaidi kwa likizo zako?

15. Ni kitu gani unapendekezea ili kuinjoy siku yako?

16. Je wewe ni mtu wa kufuga mnyama gani? Paka ama mbwa?

17. Kama ungetawala dunia, ungetaka kubadilisha kitu gani?

18. Mapenzi mazuri ni yapi kulingana na mtizamo wako?

19. Mzazi gani yuko karibu na wewe?

20. Ni kitu gani kinachokuboa kwa mwanaume?

21. Unapenda kuvalia kikazi ama kimtaa?

22. Unawachukuliaje wanawake ambao wanapenda maringo?

23. Hivi ni kweli kuwa wewe unakuwa mrembo hivi?

24. Je wewe ni mtu wa kusoma ama wapenda kucheza games?

25. Ni mtu gani katika maisha yako ambaye unampenda zaidi?

26. Unapenda mambo ya ghafla ghalfa ama mpangilio?

27. Ni nani huwa unaongea naye kama unapata changamoto katika mapenzi?

28. Je una kumbukumbu yeyote ya utotoni mwako ambayo inakufanya utabasamu unapoifikiria?

29. Ukisafiri katika hii dunia, ungetamani usikose nchi ngapi tano?

30. Ni kitu gani kinakufurahisha maishani mwako?

31. Je, wewe uko karibu na familia yako?

32. Ni kitu gani unachochukia zaidi kuona wakati unapokutana na deti wako mara ya kwanza?

33. Je wewe ni mtu wa kurauka mapema ama kuchelewa usiku zaidi?

Haya yafuatayo ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kumuuliza deti wako iwapo ameingiliana na mazungumzo yako. Maswali haya yanaweza kuwa ya ucheshi, mengine yanaweza kuchangia kuongeza mazungumzo na baadhi yanaweza kubashiri vile ambavyo deti yako itakuwa mbeleni na huyu mwanamke.

34. Ni sehemu gani ya mwili wako huwa inatekerenyeka zaidi ikiguswa?

35. Ulikuwa miaka mingapi mara ya kwanza ulipohisi kupenda mtu flani?

36. Ni kitu gani kinachofanyika kawaida unapokuwa na marafiki zako wa kike mkiwa mnapokula bata?

 37. Kimtizamo wako, maana ya mahusiano ni nini?

38. Hivi, mahusiano yako ya awali yalichukua muda gani?

39. Deti yetu ya leo umeiona vipi kabla tumeet tena wakati mwingine?

40. Sahizi unafikiria nini?