Friday, July 13, 2018
ZIJUE NJIA ASILIA ZA KUPUNGUZA UZITO KWA KUSOMA HAPA
Kabla ya kukimbilia kujinyima vyakula ili kupunguza uzito, inabidi uamue ni uzito gani unaouhitaji. Wataalamu hawashauri kushusha uzito ghafla kwa zaidi ya kilo 22 ndani ya wiki.
NJIA ZA ASILI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO:
1. Tambua Mahitaji ya Karoli(Nguvu)
Kabla hujaamua jinsi ya kula, unapaswa kufahamu ni Kalori(Nguvu) kiasi gani unahitaji kwa siku. Hii inaweza kupatikana kwa kikokotozi maalumu cha Kalori (Nguvu) kinachotumia kimo, uzito, umri na shughuli za mhusika.
2. Jifunze Kutumia Matunda na Mboga za Majani
Unahitaji walau vipande vitano vya matunda na mboga za majani. Kufanya hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu(valuable fibres) na vitamini muhimu. Pia vinajaza tumbo lako na hufanya usihitaji kula vyakula vya Kalori(Nguvu) sana.
3. Angalia Kiwango cha Chakula unachotumia
Jizuie kula vyakula vyenye Kalori(Nguvu) sana mfano maharage ya soya, mafuta ya samaki, soseji, karanga n.k na ukilazimika kula kwa kiwango kidogo sana. Dondoo ya muhimu ni kutafuna chakula chako taratibu na kwa muda unaofaa ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula na hii itakusaidia kula kidogo.
4. Usiruke Mlo!
Wengi wanaotaka kushusha uzito huona kujinyima milo mfano kuacha kula mchana au asubuhi au usiku ndio njia sahihi wakati sio sahihi, kula chakula kidogo kutafanya mwili uwe na afya. Unaweza hata kugawa ile milo mitatu mikubwa katika vijisehemu vitano au sita vya muda mfupi.
5. Matunda na Mboga Safi ya Asili ndio sahihi zaidi
Vyakula vilivyosindikwa viwandani vina sodiamu na mafuta kwa wingi. Unatarajiwa sana kushusha uzito ukitumia vyakula asili.
6. Usidhibiti sana Matumizi ya Vyakula
Unaweza kuendelea kula vyakula unavyopenda kama vipande vya keki lakini hakikisha unatumia kwa tahadhari kubwa vitu hivyo vyenye sukari ili visiwe vipingamizi vya kushusha uzito wako.
7. Usiamini kila kitu Kilichoandikwa kwenye Lebo za Vyakula
Lebo zinazosema haina mafuta haimaanishi kuwa kuna kiwango kidogo cha Kalori(Nguvu). Ni sawa na zile lebo zinazosema kiwango kidogo cha sukari(low sugar).
8. Dhibiti kiwango cha Vinywaji vya Sukari unavyokunywa
Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi
8 za maji safi na salama ambayo yatasaidia kutoa sumu na uchafu
mwilini.
9. Ainisha vyakula utakavyokula
Kuandika mpangilio wa vyakula utakavyokula kutakulinda na kuhakikisha vyakula vya kutia nguvu unavyokula ni sahihi na pia ni kikumbusho cha kila wakati juu ya ni vyakula gani unahitaji.
10. Kumbuka kufanya mazoezi siku hadi siku
Dakika 30-60 za mazoezi kila siku zitalinda afya yako na kukusaidia Kupunguza UZITO