Friday, July 13, 2018

Vipodozi Visivyo Salama/Vilivyopigwa Marufuku Na Madhara Yake


SEHEMU YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI
Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.

Hivyo hujumuisha :

  • -Vipodozi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
  • -Vipodozi vyenye viambata (kemikali) vya sumu na vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
  • -Vipodozi ambavyo muda wake wa matumizi umeisha
  • -Vipodozi ambavyo havioneshi tarehe ya kuharibika (mwisho wa matumizi)
  • -Vipodozi ambavyo maelezo yake hayajaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza

Vinaweza vikawa ni mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika.

1.1 VIAMBATA (KEMIKALI) VYA SUMU VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:

  1. Chloroquinone (Hydroquinone na kemikali zingine)
  2. Steroids (Mifano ni Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol, na Dexamethasone)
  3. Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo
  4. Chloroform
  5. Bithionol
  6. Hexachlorophene
  7. Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo
  8. Vinyl chloride
  9. Zirconium na kemikali zinazotokana nayo
  10. Methyelene chloride
  11. Halogenated salicylanilides (Dimetabromsalan, Trimetabromsalan na Tetrabromsalan)
  12. Chlorofluorocarbons (Kwenye pafyumu na deodorants)

1.2 JINSI YA KUJUA KAMA KIPODOZI KINA KIAMBATO (KEMIKALI) CHA SUMU KILICHOPIGWA MARUFUKU

Angalia kwenye lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka 12.

Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA).

Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani. Ambalo pia ni kosa kisheria.

Mifano

  1. Sabuni ya JARIBU ina kiambato MERCURY. Sabuni hii sio salama, haifai kwa matumizi na imepigwa marufuku.
  2. Losheni/krimu ya MEKAKO ina kiambato HYDROQUINONE. Losheni/krimu hizi sio salama, hazifai kwa matumizi na zimepigwa marufuku
  3. Krimu za FAIR & LOVELY SUPER CREAM, VISIBLE DIFFERENCE CREAM, SKIN SUCCESS FADE CREAM, DEMOVATE NA DIPROSON CREAM zina viambata Krimu hizi sio salama kutumika kama vipodozi na zimepigwa marufuku

SEHEMU YA PILI
2.0 MADHARA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA
Vipodozi visivyo salama vina madhara mengi sana kwa afya ya mtumiaji. Na kama mtumiaji ni mjamzito basi madhara hayo yanaweza kumpata na mtoto aliyepo tumboni.
Pia vipodozi hivi vina athari nyingi sana kiuchumi kwani vitapelekea mtu kutumia pesa tena kugharamia matibabu ya matatizo atakayopata. Madhara hayo ni pamoja na:
  • -Ugonjwa wa saratani (kansa) ya ngozi, maini, ubongo, mapafu, mfumo wa damu, utumbo mpana na kibofu cha mkojo
  • -Uharibifu wa ngozi, macho, ini, mapafu na figo
  • -Magonjwa ya moyo na kutopumua vizuri
  • -Kutokwa na chunusi kubwa kubwa
  • -Ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu na kutokwa na vipele
  • -Ngozi kuwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji, kidonda kitachelewa kupona au hakitapona
  • -Mzio (Allergy) na muwasho wa ngozi
  • -Kichefuchefu, kutapika, kusikia usingizi na kizunguzungu
  • -Magonjwa ya akili, mishipa ya fahamu (hasa kichwani)
  • -Uharibifu wa ubongo na mtindio wa ubongo kwa watoto wachanga na waliopo tumboni
  • -Ngozi kuwa laini na kusababisha kupata magonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi
  • -Kuchubuka kwa ngozi
  • -Ngozi kuwa na mabaka meusi na meupe au rangi mbalimbali
  • -Upofu, uziwi na upotevu wa fahamu wa mara kwa mara
  • -Kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
2.2 USHAURI
Kama tulivyoona hapo juu mengi ya madhara ya vipodozi visivyo salama ni makubwa na huhatarisha kabisa afya za watumiaji na watoto. Hivyo ni vyema kuvijua na kuviepuka kabisa  ili usiweze kupata madhara.
Pili msaidie kumuelimisha ndugu, jamaa na rafiki nay eye ajue na asitumie kabisa vipodozi visivyo salama
Pia ukiona mtu au duka ambalo linauza vipodozi visivyo salama acha kununua vipodozi kutoka kwake na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa
Epuka kabisa vipodozi visivyo salama. Hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.
SEHEMU YA TATU
3.0 ORODHA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA
Vifuatavyo ni vipodozi visivyo salama na vimepigwa marufuku kutumika. Epuka kabisa kutumia vipodozi hivi hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.

3.1 Krimu, Losheni na Jeli  zenye kiambato cha Hydroquinone
  1. Mekako Cream
  2. Rico Complexion Cream
  3. Princess Cream
  4. Butone Cream
  5. Extra Clair Cream
  6. Mic Cream
  7. Viva Super Lemon Cream
  8. Ultra Skin Tone Cream
  9. Fade-Out Cream
  10. Palmer’s Skin Success (Pack)
  11. Fair & White Active Lightening Cream
  12. Fair & White Lightening Cream
  13. Fair & White Strong Bleaching Treatment Cream
  14. Fair & White Body Clearing Milk
  15. Maxi-Tone Fade Cream
  16. Nadinola Fade Cream
  17. Clear Essence Medicated Fade Cream
  18. Peau Claire Body Lotion
  19. Reine Clair Rico Super Body Lotion
  20. Immediate Claire Maxi –Beauty Lotion
  21. Tura Lotion
  22. Lkb Medicated Cream
  23. Crusader Skin Toning Cream
  24. Tura Bright & Even Cream
  25. Claire Cream
  26. Miki Beauty Cream
  27. Peau Claire Crème Eclaircissante
  28. Sivoclair Lightening Body Lotion
  29. Extra Clair Lightening Body Lotion
  30. Precieux Treatment Beauty Lotion
  31. Clear Essence Skin Beautifying Milk
  32. Tura Skin Toning Cream
  33. Madonna Medicated Beauty Cream
  34. Mrembo Medicated Beauty Cream
  35. Shirley Cream
  36. Kiss – Medicated Beauty Cream
  37. Uno21 Cream
  38. Princess Patra Luxury Complexion Cream
  39. Envi Skin Toner
  40. Zarina Medicated Skin Lightener
  41. Ambi Special Complexion
  42. Lolane Cream
  43. Glotone Complexion Cream
  44. Nindola Cream
  45. Tonight Night Beauty Cream
  46. Fulani Cream Eclaircissante
  47. Clere Lemon Cream
  48. Clere Extra Cream
  49. Binti Jambo Cream
  50. Malaika Medicated Beauty Cream
  51. Dera Heart With Hydroquinone Cream
  52. Nish Medicated Cream
  53. Island Beauty Skin Fade Cream
  54. Malibu Medicated Cream
  55. Care Plus Fairness Cream
  56. Topiclear Cream
  57. Carekako Medicated Cream
  58. Body Clear Cream
  59. A3 Skin Lightening Cream
  60. Ambi American Formula
  61. Dream Successful
  62. Symba Crème Skin Lite ‘N’ Smooth
  63. Cleartone Skin Toning Cream
  64. Ambi Extra Complexion Cream For Men
  65. Cleartone Extra Skin Toning Cream
  66. O’nyi Skin Crème
  67. A3 Triple Action Cream Pearlight
  68. Elegance Skin Lightening
  69. Clere Cream
  70. Clear Touch Cream
  71. Crusader Ultra Brand Cream
  72. Ultime Skin Lightening Cream
  73. Rico Skin Tone Cream
  74. Baraka Skin Lightening Cream
  75. Fairlady Skin Lightening Cream
  76. Immediate Claire Lightening Body Cream
  77. Jaribu Skin Lightening Lotion
  78. Amira Skin Lightening Lotion
  79. A3 Clear Touch Complexion Lotion
  80. A3 Lemon Skin Lightening Lotion
  81. Kiss Lotion
  82. Princess Lotion
  83. Clear Touch Lotion
  84. Super Max-Tone Lotion
  85. No Mark Cream
  86. Body Clear
  87. Top Clear
  88. Ultra Clear
  89. Peau Claire Lightening Body Oil
  90. G &G Dynamiclair Lotion
  91. G & G Teint Uniforme
  92. G & G Cream Lightening Beauty Cream
  93. Dawmy – Lightening Body Lotion
  94. Maxi White Cream
  95. Bioclare Lightening Body Lotion
3.2 Vipodozi vingine vyenye Hydroquinone
  1. Fair & White Powder (Exclusive Whitenizer & Serum)
  2. New Youth Tinted Vanishing Cream
  3. Skin Success Fade Cream Regular
  4. Teint Clair Clear Cpmplexion Body Lotion
  5. Mareme Cream
  6. Si Clair Plus Cream
  7. Clair & White Body Cream
  8. Body White Lotion
  9. Bio Claire Cream
  10. Forever Aloe MSM Gel
  11. Kroyons Baby Oil
3.3 Sabuni zenye kiambato cha Hydroquinone
  1. Body Clear Medicated Antiseptic Soap
  2. Blackstar
  3. Cherie Claire Body Beauty Lightening & Treating Soap
  4. Immediate Claire Body Beauty Soap
  5. Lady Claire
  6. G.C Extra Clear
  7. Top Clear Beauty Complexion Soap
  8. Ultra Clear
3.4 Vipodozi vyenye Hydroquinone pamoja na Steroid
  1. Clear Essence Skin Beautifying Milk For Sensitive Skin
  2. Fair & White Clarifiance Fade Cream
  3. Fair & White Exclusive Whitenizer Body Lotion
  4. Fair & White Exclusive Whitenizer Cream
  5. Fair & White Exclusive Whitenizer Gel
  6. Fair & White Maxitone Lightening Lotion Sun Block
  7. Fair & White So White Skin Perfect Gel
3.5 Sabuni zenye kiambato cha Mercury (Zebaki) na michanganyo yake
  1. Movate Soap
  2. Miki Soap
  3. Jaribu Soap
  4. Binti Jambo Soap
  5. Amira Soap
  6. Mekako Soap
  7. Rico Soap
  8. Tura Soap
  9. Acura Soap
  10. Fair Lady
  11. Elegance
  12. Block & White Skin Whitener Germicidal Bath Soap
  13. Rose Beauty Soap
  14. Maxi-Tone Soap (Skin Lightening Soap)
  15. Margostara Soap (New Tannin)
  16. Rusty – Whitening Soap (New Formula)
  17. Emani Natural Fair Pearls Soap
3.6 Krimu zenye kiambato cha Mercury na michanganyiko yake
  1. Pimplex Medicated Cream
  2. New Shirley Medicated Cream
3.7 Krimu zenye Steroids (Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol,
Dexamethasone nk)
  1. Amira Cream
  2. Jaribu Cream
  3. Fair & Lovely Super Cream
  4. Neu Clear Cream Plus (Spots Remover)
  5. Age Renewal Cream
  6. Visible Difference Cream (Neu Clear Spots Remover)
  7. Body Clear Cream
  8. Sivo Clair Fade Cream
  9. Skin Balance Lemon Cream
  10. Peau Claire Cream
  11. Skin Success Cream
  12. M & C Dynamic Clair Cream
  13. Skin Success Fade Cream
  14. Fairly White Cream
  15. Clear Essence Cream
  16. Miss Caroline Cream
  17. Lemonvate Cream
  18. Movate Cream
  19. Soft & Lovely Cream
  20. Mediven Cream
  21. Body Treatment Cream (Spots Remover)
  22. Dark & Lovely Cream
  23. Sivo Clair Cream
  24. Musk – Clear Cream
  25. Fair & Beautiful Cream
  26. Beautiful Beginning Cream
  27. Diproson Cream
  28. Demovate Cream
  29. Top Lemon Plus
  30. Lemon Cream
  31. Beta Lemon Cream
  32. Tenovate Cream
  33. Unic Clear Super Cream
  34. Topifram Cream
  35. First Class Lady Cream
3.8 Vipodozi vingine vyenye kiambato cha Steroid
  1. Fashion Fair Gel Plus
  2. Hot Movate Gel
  3. Hyprogel
  4. Mova Gel Plus
  5. Secret Gel
  6. Secret Cream
  7. Peau Claire Gel Plus
  8. Hot Proson Gel
  9. Skin Success Gel Plus
  10. Skin Clear Gel Plus
  11. Soft & Beautiful Gel
  12. Skin Fade Gel Plus
  13. Ultra – Gel Plus
  14. Zarina Plus Top Gel
  15. Action Demovate Gel Plus
  16. Prosone Gel
  17. Skin Balance Gel Wrinkle Remover
  18. TCB Gel Plus
  19. Demo – Gel Plus
  20. Regge Lemon Gel
  21. Ultimate Lady Gel
  22. Topifram Gel Plus
  23. Clai & Lovely Gel
  24. Fair & White Serum Exclusive Whitenizer
  25. Maxi White Lightening Body Milk
  26. Maxitone Cleansing Milk
  27. Avoderm Cream
  28. Niomre Cream
  29. Niomre Lotion
  30. Nyala Lightening Body Cream
  31. Si Clair Cream
  32. Cute Press White Beauty Lotion
  33. White SPA Rose Lotion
  34. White SPA UV Lightening Cream
3.9 Vipodozi vya kupunguza unene vilivyopigwa marufuku
  1. Bio Valley Sliming Gel
3.10 Vipodozi vya nywele vilivyopigwa marufuku
  1. African Gold Super Glo
  2. Sofn Free Hair Foodblue Cap Shampoo
  3. Marhaba Anti-Dandruff Hair Cream
  4. Blue Cap Spray
  5. Blue Cap Cream
3.11 Vipodozi vinginevyo vilivyopigwa marufuku
  1. Bio Light Cream
  2. Salon Dermaplex Amazon Clay 9Normal To Dry Skin)
  3. Beauty Secrets Body Cream
  4. Swiss Soft N White Lightening Gel
  5. Whitening Complex Mask
3.12 Vipodozi Vinavyosababisha muwasho vikitumika karibu na macho
  1. Eye Shadow Gel
  2. Eye Shadow Gel 02
  3. Eye Shadow Gel 07
  4. Eye Shadow Gel 08
  5. Eye Shadow Gel 09
  6. Eye Shadow Gel 10
TAHADHARI :  VIPODOZI VISIVYO SALAMA VIPO VINGI ZAIDI YA HIVYO AMBAVYO VIMEORODHESHWA HAPO JUU NA VINGINE VINGI ZAIDI VINAWEZA VIKAFIKA SOKONI.
Mara zote kuwa makini na vipodozi na pata taarifa, elimu na ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wataalam wa afya, urembo na vipodozi.