Friday, July 13, 2018

TOFAUTI YA KUFIKA KILELENI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME

Wanaume hufurahia sana kufika kileleni.
Hata kama ni sekunde chache hata hivyo zinalipa zaidi kuliko raha ya hekaheka zote hadi kufika hapo. Ni kweli kwamba mwanaume na mwanamke ni tofauti sana linapokuja suala la kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa.
Mwanamke anaonekana ndiye mwenye uwezo zaidi wa kuwa na wakati mrefu wa kukaa kileleni na pia ana uwezo wa kujirudia kufika kileleni zaidi ya mara moja.
Pia inaeleweka wazi kwamba ni rahisi sana kwa mwanaume kufika kileleni kuliko mwanamke kwani ni wanawake wengi ambao pamoja na kushiriki tendo la ndoa bado hawajawahi kufika kileleni wakati itakuwa gumzo ikitokea kwamba kuna mwanaume ameshashiriki tendo la ndoa na hajawahi kufika kileleni, hayupo!
Pia mwanamke anao uwezo wa kudhibiti kufika kileleni, hata kama mwanaume ataweza kudhibiti kumaliza mapema (ejaculate) kabla hajafikia point ya no return, hata hivyo akishafika hiyo point hawezi kusimama au kugoma asifike kileleni.
Wakati huohuo mwanamke anaweza kuwa alikuwa kileleni na akasikia mtoto analia, anaweza kuacha na kumhudumia mtoto na kuanza kila kitu upya.
Tofauti nyingine katika kufika kileleni kwa mwanaume na mwanamke ni wakati kwa maana kwamba kwa mfano mume amesafiri kwa wiki mbili kwa ajili ya business, mwili wa mwanamke huweza kujizima kiaina kwa sababu hayupo sexual active na atahitaji muda zaidi kuupasha mwili kuwa tayari kwa sex na hatimaye kufika kileleni.
Mwanaume kwa upande mwingine ni kinyume na mwanamke, kama hakuwa na sex kwa wiki mbili basi mwili wake utajaza risasi za uhakika na siku akikutana na mke wake hatachukua muda kufika kileleni, kwanza ile kumuwaza mke wake tu tayari Uume unaanza kufanya vitu vyake (erections).
Jambo la msingi ni mume na mke kufahamu tofauti zilizopo na kuzifanyia kazi ili kusherehekea kitendo cha kuishi pamoja.