Friday, July 13, 2018

Je, unaijua chemchem ya ujana (the fountain of youth)?

hello,
Tumerudi tena kwenye yale mambo mazuri ya kushirikishana.πŸ˜‰
Wanawake wengi baada ya kufika umri fulani hujihisi wanapoteza urembo wao na uwezo wa kuwa wenye nguvu na wachangamfu, na wengine hufikia hata kudanganya umri wao. Wngine wanaita Middle age Crisis nk.
Ukweli ni kwamba ujana ni mtamu.πŸ‘§

Tatizo kubwa ni kwamba ujana hautumiwi vema, kuweza kuutunza ujana ndo dawa.
DOWNLOAD APP YA SMS ZA MAPENZI. BONYEZA HAPA

Sasa Tufanyaje

1. Aina za Vyakula

Ni vema kadri umri unavoenda mtu abadilishe aina ya vyakula anavyopendelea, Kutokana na mifumo ya mwili kuendelea kubadilika kutokana na umri mwili hautaweza tena kumeng'enya baadhi ya vyakula. Hali ya kuulazimisha mwili ufanye kazi sana katika kusaga chakula unachokula inaweza kuwa moja ya sababu muda mwingi mtu anakuwa anajisikia amechoka na kufubaa.
Baadhi ya vyakula ambavyo umeng'enyaji wake huweza kuwa mgumu ni Nyama, baadhi ya vyakula vya wanga (vya ngano) na kwa wengine maziwa. sio kwamba uache kabisa maana kuna faida nyingi kwenye vyakula hivi, ila kuvitumia mara chache na kwa kiasi.
Kadri umri unavyoenda ni vema tukapunguza ulaji wa vyakula hivi pia kuwa na mpangilio mzuri wa kula, yaani ratiba maalumu sio tu unakula muda wowote; ili kuupa mwili nafasi ya kusaga chakula na kukisambaza kifanye kazi.
Vyakula vingine vinaleta madhara kutokana na aina ya uandaaji, mfano viazi badala ya kukaanga kwenye mafuta unaweza kuchemsha ukatia viungo na mafuta kwa mbali na ukafurahia mlo wako, akaoka kwenye oven hata samaki au yai badala ya kukaanga ukachemsha.
Vitamin na madini ni muhimu mwilini hakikisha hukosi.
say bye to junk foods πŸ‘‹

2.Maji
Hili halikwepeki, ni vema kunywa maji mengi kila siku ili kuwezesha mifumo ya mwili kufanya kazi sawasawa, wingi wa maji unategemea pia uzito wa mwili wako. usinywe tu pale unapojisikia kiu unaweza kunywa badala ya vinywaji unavyopendelea kama soda nk. wataalamu wanasema unahitaji maji asilimia 67 ya uzito wako.

3.Urahisishie mwili wako kazi
Pamoja na kwamba mwili wa binadamu una namna nyingi ya kuweza kujilinda na kutekeleza majukumu yake ila ni vema usiuongezee mzigo ili kujipa msaada usizeeke haraka. Hakikisha unarahisisha mmeng'enyo wa chakula unachokula kwa kujitahidi kula mboga za majani, kachumbari, matunda na nafaka zisizokobolewa. Namna hii utaupa mwili urahisi wa kudhibiti sukari mwilini na kuweza kufanya chakula kipite vizuri na upate choo sawasawa. 

4.mazoezi
Wengi tumekuwa wahanga wa starehe ya kazi za kukaa na magari, kutembea kidogo kidogo inaweza kuwa msaada kwa mwili, inasaidia kuweza kudhibiti mafuta mabaya na kuchangamsha mwili hata mmeng'enyo wa chakula unaenda vizuri.

5.mtazamo
Kadri siku tulizoishi zinavyo ongezekana kuna mambo mengi tunakuwa tumekutana nayo, kuna yale ya kuumiza na kuna yale yaliyotokea na ambayo tuna wasiwasi yanaweza kutokea. Kuwa na wasiwasi hakubadili ukweli wa jambo, na kuendelea kuwaza jambo ambalo limeshatokea hakubadilishi ukweli kwamba limetokea. Hivyo ni vema yale mambo tusiyoweza kuyabadilisha tuyaache na tuhangaike na kuwaza πŸ’­ kuhusu yale yanayoweza kubadilika.
furahia kila siku unayoamka asubuhi maana kwa kuwa uko hai bado kuna tumaini. Ni vema kudhibiti mawazo hasi kwa faida ya afya  ya mwili.
6.kupumzika vya kutosha
Pata muda wa kutosha kuweza kupumzika, kukosa usingizi ni moja ya mambo yanayozeesha bila mtu kujua unastuka tu mng'ao wa ngozi umepotea, akili haina uwezo kama awali na una dark circles machoni !
inashauriwa mtu aweze kulala masaa 8, ila angalau masaa 6 mtu usikose maana tafiti mpya zinaonesha kukosa usingizi kunaongeza uwezekana wa kupata magonjwa ya moyo maradufu ukiachia kuzeeka mwili.

7. Punguza Matumizi ya vilevi
kadri unavyokuwa na umri mkubwa ni vema ukapunguza vilevi, vilevi hupunguza maji mwilini na bila maji ngozi yako inazeeka. Pamoja na kupoteza maji pia unachakaza baadhi ya viungo vya ndani hasa vyenye kazi ya kuvhuja taka mwili na sumu, pia pombe huvuruga sukari ya mwili wako hivyo kuvuruga utendaji kazi wa mwili.
unywaji kwa kiasi tu,sio kupania ila ni vema ukapunguza mpk kuacha kabisa.
 Kuna watu wanaonekana wazee kuliko umri wao kwa sababu tu ya ulevi wa pombe.
8.JipendeπŸ’–
Kujipenda kunajumuisha mambo mengi ndani ikiwemo kutojipa stress, kutonung'unika watu wasipokutendea ulivyotegemea na zaidi jigharamie kwa vitu vizuri, check ups za afya na kujitendea mambo mazuri.
Usikae unajikumbusha mambo mabaya yaliyokuumiza, fanya vitu vinavyokupa wewe faida, usiende an extra mile kwa ajili tu ya kufurahisha watu wakati wewe unadhurika.
Make money and spend money on what u need, that's why we make money.😎

9. Matumizi yaVipodozi
Anza mapema kuepuka vipodozi vikali, vipodozi vingi vyenye ukali huichosha ngozi na ni ukweli usiofichika hata katika uzee ngozi yako itaonekana tu kwamba enzi hizi ilipitia mapito magumu. 😐
Unaweza kuangalia post mbalimbali za treatment/ vipodozi natural na vya kuusubirisha uzee humu humu. Unaweza kutumia anti-aging products, ila lifestyle ndio option namba moja.

10. Jua
Miale mikali ya jua ni moja ya vitu vinavyozeesha, kuna watu husema wafanyakazi wa maofisini au Bank huwa hawazeeki haraka mara wanajipenda mno ndo maana hawazeeki n..k ila moja ya factor ya wao kuonekana na ngozi nzuri muda mrefu ni kutopata miale ya jua muda mrefu, muda mwingi watu hao huwa wako ndani ni ngumu kupatwa na jua la kuzeesha... ila iwapo unalazimika kutembea juani, basi tumia sunscreen spf yoyote ila kama ni mji wa jua kali sana basi tafuta hata ya spf 30 kuendelea.



Hakuna uchawi wala location ya maji ya ujana, ni kujifanyia hayo tu.