Tuesday, May 8, 2018

SABABU KUMI ZA MIGOGORO KATIKA NDOA AU MAPENZI

Ingawa tufunga ndoa na kuamua kuishi pamoja, lakini tunakumbana na mengi, kuna yaliyondani ya uwezo wetu kuyatatua na kuyaondoa kabisa, lakini kuna mengine yapasa tupate msaada toka kwa wanaotuzunguka na wenye nia njia na mahusiano yetu na ndoa zetu kwa ujumla.Kwa uchache nizielezee sababu zinachangia migogoro katika ndoa nyingi, ukizijua utajitahidi katika ndoa yako sizikukute au kama mshakumbana nazo, mzifahamu na mjue jinsi ya kuzikabili.

1.Matatizo ya Kifedha
Pengine hii ndio huwa sababu kubwa mara nyingi, na hasa inapotokea wakati mnaoana hali ya kifedha ilikuwa nzuri tu, lakini sasa mambo yamebadilika kidogo na gharama za maisha zimekuwa juu!

2. Watoto.
Ingawa kabla ya kuwapata mlikuwa mnahamu na mnawaomba kila kukicha, lakini mara nyingi watoto huja na changamoto zao kikubwa ni kupunguza map#nzi baina yenu hasa wakiwa wachanga au wakiwa ndo kwanza wanakua kua.

3. Kufanya Map#nzi
Hapa napo panachangia mno. Inawezekana ikawa kiwango cha map#nzi, ladha ya map#nzi au ufundi na utundu, umepungua au umeisha kabisa. Wakati mwingine ni map#nzi ya mgao kama umeme vile kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo U Busy wa wanandoa hasa wafanya kazi.

4.Kuwa Mbali Mbali
Hii nayo huchangia hasa mwenza anapokuwa anafanya kazimbali nawe, au muda mwingi anakuwa mbali nawe kutokana na mazingira yake ya kazi, mathalani mwana usalama au mkurugenzi fulani.

5.Majukumu ya Nyumbani
Hili huwagusa zaidi wanandoa ambao wote ni waajiriwa au wanajishughulisha kitofauti tofauti na hivyo basi kila mmoja ana uwezo binafsi wa kipato. Nani afanye nini? Lipa Ada ya wototo, mimi nilipe kodi ya nyumba!

6.Marafiki
Si katika wote miongoni mwa marafiki tulionao ni wema kwetu. wengine huliangalia p#nzi letu kwa husuda na wanatamani kila leo tuwe tumeachana, ingawa hawalitamka hilo mdomoni lakini wanaweza kujionesha kwa vijitabia vyao na maneno yao.

7.Kulinganisha Tabia
Inawezekana ulikuwa katika mahusiano fulani kabla ya haya uliyonayo sasa au kabla ya ndoa yako. Kama ni hivyo usiwe na mazoea ya kulinganisha au kupisha mambo ya Mp#nzi wako wa zamani na mumeo/Mkeo wa sasa, hii itakufanya ushindwe kusonga mbele hasa mkigombana au kuudhiana kidogo na kuanza kusema "Enzi za Fulani, angenifanyia hivi..."

8. Familia.
Ndugu, Jamaa na watoto wetu, au watu wetu wa karibu huwa miongoni mwa sababu za kuvunjika mahusiano na ndoa zetu kwa ujumla. Watoto wa kambo, mawifi na mashemeji. Inabidi tuwaweke Wake/Waume zetu kwanza kabla ya wote ili tuwe na nguvu ya pamoja katika kutatua matatizo yanayotusibu.

9. Matarajio.
Kuna Baadhi yetu huwa tunaingia katika ndoa tukiwa na matarajio mengi na hali inakuwa tofauti tukashaingia ndani ya ndoa. Tutafanyaje? kwa wenye mwepesi huwa hawadumu na kusema bora tuachane tu, Mbona wakati nipo Single mambo yalikuwa safi tu. Ila kwa wachache huweza kustahimili na kukubali kile kilichokuwa mbele yao, na hatimaye kukishinda.


10 Migogoro Binafsi.
Kamwe tusiruhusu migogoro yetu binafsi iwe ya kazini au wapi ambayo haina mahusiano na ndoa zetu ikaharibu ndoa zetu. Hata kama wamekutibua ofisini hasira zako ziache mlangoni na uingie kwa Mumeo/Mkeo ukiwa na tabasamu kama ndo mmetoka kuoana.

Kwa machache haya naimani tutayaangalia kwa mtazamo mpana zaidi na kuyafanyia kazi, ili tuzidi kuishi na mahusiano yetu vizuri na ndoa zetu kwa ujumla.

Nakaribisha Maoni yako Mdau wangu......!!!!