Friday, April 27, 2018

ZIFAHAMU NJIA KUMI ZA KUFANYA MACHO YAKO YAWE MEUPE SANA.

eneo la ndani la jicho ambalo hua ni jeupe kitaalamu linaitwa sclera, weupe wa eneo hili ni dalili nzuri kwamba mtu fulani yupo safi kiafya, kiurembo na kiakili. eneo hili likiwa njanoa au nyekundu sio dalili nzuri huenda ikawa ni ugonjwa wa maini, allergy ya macho, sumu nyingi mwilini au magonjwa mengine mbalimbali lakini pia hukufanya uonekane mzee hata kama ni binti mdogo au kijana mdogo.watu maarufu hasa wa nje ya nchi huonekana na macho meupe sana lakini ile hua sio bahati ila kuna mambo wanazingatia kua vile na leo naenda kuyazungumzia kama ifuatavyo.
kutumia matone yakusafisha macho; kuna matone ya macho maalumu mfano clear eyes eye drops ambayo unakua unaweka machoni angalau kutwa mara nne mpaka dalili zote zitakavyopotea.matone haya huondoa miwasho na ukavu wa macho na kuyaacha yakiwa na unyevunyevu.
kula matunda na mboga za majani; vitu hivi vina vitamin muhimu kwa ajili ya macho mfano a,c, na e ambazo kimsingi ndio muhimu sana kwa ajili ya macho.vyakula hivi pia huisaidia maini kua kuondoa sumu mwilini.maini yenye afya hufanya kazi vizuri na kuusaidia mwili kirahisi.
                                                           
pata usingizi wa kutosha; binadamu anatakiwa alale angalau masaa saba mpaka nane kwa siku ili kuurudisha mwili uliochoka katika hali yake ya kawaida; ukichunguza mtu aliyekosa usingizi hata siku moja hua na macho mekundu sana sababu ya uchovu mkali.
                                                 
kunywa maji mengi sana; unywaji wa angalau glass 8 mpaka kumi kwa siku ni muhimu sana kwa macho yako kwani maji husafisha mwili wote na kuondoa sumu pia kuondoa uvimbe wa macho ambao hutokea mtu anapotoka kuamka tu.kutokunjwa maji kutaufanya mwili uwe mkavu na macho mekundu.
acha pombe na kahawa; vyote hivi hupunguza sana maji mwilini kwa kukufanya ukojoe mara kwa mara lakini pia hufanya macho kuvimba na kuharibu mfumo wako wa kulala kwa kukosa usingizi sababu ya kahawa na kulala sana sababu ya kunywa pombe.
kaa mbali na moshi na vumbi; vitu hivi siku zote vikiingia machoni huleta machozi na kusababisha machozi mengi. sasa hali hii kwa macho so nzuri kwani itakufanya uwe na macho  mekundu sana.lakini pia usivute sigara au kukaa karibu na watu wanaovuta sigara.
                                                 
vaa miwani ya jua kipindi cha jua kali; mara nyingi hua tunaona wazungu wanavaa miwani nyeusi na hua hatuelewi ni kwanini tunahisi labda ni urembo tu na ukimuon mweusi mwenzako amevaa unahisi anataka kua sharobaro tu. miwani nyeusi inatukinga na miale ya jua kitaalamu kama utra violet light ambayo hutengeneza mtoto a jicho iwapo miale hiyo ikikupata kwa muda mrefu.ni vizuri kuivaa kwenye jua kali kukinga macho.
                                                       

tumia virutubisho; kwa sasa kuna virutubisho vingi sana ambavyo vina kila chakula ambacho macho yanakihitaji kua safi yaani vitamin zote muhimu za macho.virutubisho hivi husaidia kua na macho meupe, husaidia kuona kwa watu wenye umri wa miaka 40 ambao macho yao huanza kuishiwa nguvu na kushindwa kusoma vitu vya karibu bila kuvaa miwani lakini pia ni vizuri kwa matatizo mbalimbali ya macho.tunaweza kuwasiliana ukavipata.
punguza kazi za macho; watu wanaofanya kazi kwenye computer au kungalia movie au miziki siku nzima wanachosha sana macho na kuyafanya kua mekundu ni vizuri kua makini na hili. kama ni lazima ufanye kazi hizi basi punguza mwanga mkali wa computer na pata mwanga wa kutosha kutoka chumba unachotumia.ni hatari sana kutumia computer,simu au tv gizani.
muone daktari; kitaalamu kila mtu anatakiwa amuone daktari wa macho anagalau mara mbili kwa mwaka haijalishi kama anaumwa au haumwi.hii itakusaidia sana kugundua magonjwa ambayo yako njiani au yameanza hujagundua.
mwisho; kuna njia za asili za kusafisha macho mfano kuweka kitambaa cha baridi juu ya macho huku ukiwa umeyafunga, hii hupunguza damu nyingi kwenye macho na kuyafanya meupe.
macho ndio kila kitu katika mwili wa binadamu, ukishindwa kuona basi maisha yako yaliyobaki duniani yatakua magumu sana.