Wednesday, April 25, 2018

UFAHAMU UGONJWA WA KASWENDE NA MATIBABU YAKE. [SYPHILIS ]


kaswende ni nini?
huu ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kutoka kwa njia ya ngono au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
utafiti unaonyesha kwamba asilimia 2 mpaka 20 ya akina mama wanaoenda kupimwa kipindi cha ujauzito hukutwa na kaswende lakini pia ugonjwa huu umetapakaa sana maeneo ya mijini ukilinganisha na vijijini.

jinsi ugonjwa unavyosambaa.

  • husambaa kwa zinaa kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke
  • husambaa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.
  • mgonjwa mwenye vidonda anaweza kuambukiza mtu kwa kumkumbatia tu.
  • kugusa vidonda vya mgonjwa kwa bahati mbaya.

dalili za kaswende

  • kidonda kisichokua na maumivu hutokea baada ya siku 10 mpaka 90 baada ya kupata maambukizi, kidonda hicho hakina maumivu na hukaa siku chache na kupotea bila matibabu. kidonda hiki hutokea pale wadudu walipoingilia yaani huweza kua kwenye uume,uke, mdomoni, kwenye maziwa na kadhalika.
  • upele hutokea baada ya miezi sita na kusambaa sehemu za uke, kwenye mkundu, mikononi, miguuni, kifuani, mgongoni na hata usoni. upele huu hauwashi na kipindi hichi mgonjwa anakua hatari sana kwani huweza kuambukiza mtu kwa kumkumbatia au kumshika tu.
  • baada ya mwaka mpaka miaka kumi ugonjwa huu huingia ndani ya mwili na kushambulia mishipa ya fahamu na ubongo.mgonjwa huanza kuonyesha dalili za ugonjwa wa akili na wakati mwingine mtu hua kichaa kabisa.
vipimo vya maabara kugundua kasendwe
kipimo maalumu kitaalamu kama rapid plasma reign, kipimo hiki huweza kugundua ugonjwa wiki ya 6 mpaka 8 baada ya kuambukizwa.

matibabu
sindano maarufu kama pena du au benzathine penicilin huchomwa kwa kiasi cha 2.mu yaani 1.2m.u kwa kila tako. sindano hiyo huchomwa mara moja kwa kaswende inayoanza au mara moja kwa wiki moja kwa muda wa wiki tatu.
kwa wagonjwa wenye allergy na penicilin kuna dawa kama doxycline ambayo hutumika lakini pia kwa sasa kuna dawa nyingi mpya sokoni ambazo huweza kutumika pia mfano cefriaxon.

madhara ya kaswende

  • ugonjwa huu unaongoza kwa kusababisha kuharibika kwa mimba kuliko magonjwa mengine yoote ya zinaa, ni vizuri kwa mama kupima ugonjwa huu kabla ya kuamua kubeba mimba.
  • ugonjwa huu hauzuiliki hata kwa kondom kwani una uwezo wa kupita hata kwenye ngozi isiyo na michubuko......unaweza kusoma blog yetu ya kingereza hapa.