Monday, April 23, 2018

Nguvu ya Vitu Vya Asili Katika Ngozi Yako , ASALI., MDALASINI,

kama wewe unapenda urembo  na unaijali ngozi yako basi unaweza kutumia vitu vya asili badala ya vile vyenye madhara ambavyo vinaweza kudhuru ngozi yako .na vitu vya asili unavyoweza kutumia ni  kama mayai,mdalasini na asali huweza kukupa mn'garo mzuri lakini zaidi sana kwa wale wanaoupinga uzee mchanganyiko huo huweza kunyanyua uso wako na kuondoa mikunjo. wenyewe wanaita face lift. hebu nikupe vitendea kazi na mwisho nikupe namna ya kufanya.



                                                                           Asali

                                                               mdalasini




                                                                     Mayai

sasa! unachotakiwa kufanya ni hivi, unachukua ute wa mayai,maji ya limao ama ndimu kijiko kidogo, unga wa mdalasini kijiko kidogo,sukari kiasi na mafuta ya olive oil kijikom kidogo. changanya  pamoja na baada ya kuchanganya pakaa kwenye viwiko vya mikono, unaweza kupakaa midomo yao na usoni kwa ujumla kaa nayo mpaka itakauka, usisugue ondoa kwa kitambaa laini chenye maji ya baridi ,ukisha ondoa yote vizuri unaweza kunawa vizuri kwa maji safi na utakua tayari endapo utahitaji kutoka ama kupaka make up. jaribu uone , dada Lisa Rinna hapa chini ni shuhuda wa mchanganyo huo.