Monday, April 30, 2018

JINSI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO YAWE MEUPE ZAIDI UKIWA NYUMBANI TU.

meno ni afya, mtu ambaye ana meno mabavu kikawaida hua hana afya nzuri na huteseka sana hasa wakati anapopata maumivu makali ya meno. lakini pia meno ni moja ya sehemu za mwili za urembo kwani mtu mwenye meno meupe sana hupendeza akitabasamu kuliko mwenye meno yenye unjano kwa mbali. kila mtu anatamani kua na meno meupe sana lakini kuna sababu mbalimbali zinazuia watu kufikia malengo hayo. leo tutaona jinsi ya kufanya meno yawe meupe sana, lakini siongelei meno ya watu wa arusha, moshi na manyara mabayo yameunguzwa na madini fulani hapana yale hayatibiwi kwa njia hii na hata ukisema uyatibu kwa njia yake yanapungua upana wake na kua rahisi kuvunjika muda wowote. naongelea meno ya watu wa kawaida ambao utotoni kama kawaida ya watu wote yalikua meupe lakini kwa sasa yamebadilika rangi.

vitu vinavyohitajika,

  • hydrogen peroxide mouth wash[inapatikana kwenye maduka ya madawa]
  • maji masafi.[nunua ya dukani]
  • mswaki
  • dawa ya meno nzuri.
jinsi ya kufanya.
  • nunua chupa ya hydrogen peroxide mouth wash, kisha changanya kiasi na maji masafi kwa uwiano sawa. yaani ile chupa ya dawa kama mils 100 hivyo changanya na mils 100 za maji.
  • baada ya mchanganyiko huo weka mdomoni kiasi cha mils 30[sawa na vijiko vitatu vya kulia chakula]. sukutua mdomoni kwa dakika moja kisha utahisi povu linatokea mdomoni hapo utajua dawa infanya kazi kwani kikemia dawa hiyo ikikutana na bacteria wamdomoni inatengeneza povu.
  • tema mchanganyiko wa mdomoni kisha safisha na maji ya kawaida tu baada ya hapo piga mswaki sio chini ya dakika tano ukisugua sehemu zote za meno yaani ya mbele ya nyuma na katikati, watu wengi hupiga mswaki dakika moja tu kitu ambacho ni makosa.
  • tumia dawa hii kila siku asubuhi tu mpaka utakapoona umeridhika na matokeo na hakuna madhara yeyote ya kutumia dawa hii.
njia nyingine ukishindwa hiyo hapo ya dawa; nunua dawa ya meno ya forever living toothpaste na iwe dawa yako kila siku maishani mwako na utaona mabadiliko kwani hung'arisha meno, huleta harufu nzuri mdomoni, huzuia kuoza meno na ni dawa bora kwa sasa kuliko dawa zote za meno zinazotangazwa dunia nzima kwani haina kemikali hata kidogo. na kama wewe ni mjasiriamali hii ni fursa kubwa, unaweza ukajiunga na kampuni ili uuzie wengine unaowapenda wawe kama wewe na kupata bidhaa zingine bora za kampuni hii ambayo mwaka jana iliongoza kwa mapato makubwa katika biashara za mtandao duniani.
mambo muhimu ya kuzingatia..
epuka kutumia vyakula vinavyoyapa rangi meno yako;  yaani kama soda, chai, red wine, kahawa na kuvuta sigara. unaweza kutumia soya kuweka kwenye chai badala ya majani ya chai.
piga mswaki mara mbili kwa siku; piga mswaki asubuhi na jioni baada  ya chakula na sio kabla ya chakula kama watu wengi wanavyofanya. kulala bila kupiga mswaki husababisha vyakula vilivyoko mdomoni kushambuliwa na bacteria usiku  na matokeo yake mtu hutoa harufu kali asubuhi. watu wanaopiga mswaki usiku hua hawanuki mdomo asubuhi.
kula vyakula vya asili; matunda kama karoti, maepo, machungwa, na kadhalika husaidia meno sana kutoa mabaki ya uchafu kuliko kula nyama kia siku ambazo huacha mabaki kwenye meno. vyakula vyote vyenye sukari nyingi kama keki, pipi, ice cream,chocolate, biskuti na kadhalika sio vizuri kuvitumia kwani ni hatari sana kwa afya ya meno na rangi ya meno yako.
toa uchafu katikati ya meno; kuna kamba nyembamba sana maalumu kwa meno, hutumika kitaalamu kutoa uchafu wa meno, hizo ni nzuri sana kuliko hizi toothpick zinazotumika na watu wengi.
onana na daktari wa meno; kawaida hautakiwi kwenda hospitali wakati unaumwa meno tu, ila unatakiwa uende umuone daktari wa meno angalau mara nne kwa mwaka ili aweze kugundua tatizo lolote la meno lililoanza bila wewe kufahamu, hivyo usisubiri ukose usingizi nduio uende hospitali.