Monday, April 30, 2018

HIVI NDIVYO MWANAMKE ANAVYOWEZA KUBEBA MIMBA SIKU YA HEDHI.


Wengi najua mmeshangaa sana kuona hii post lakini huo ni ukweli mchungu unaofanya watu wanakana watoto na kuacha ndoa zao kwa kudhani wamesalitiwa wakati mimba ni zao na watoto ni wa kwao wenyewe.
Kwenye blog hii nimeshaongelea zaidi ya mara mbili mambo haya ya kuhesabu siku zako za hatari lakini hili sikulizungumzia, basi hebu twende sawa upate kunielewa vizuri na kama hukusoma hizo za nyuma na hujui kuhesabu siku zako za hatari soma hapa


Nilisema kwamba wanawake wote, siku yao ya hatari ya kubeba mimba ni siku ya 14 kabla ya kuona mzunguko unaofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita kama mnavyodanganyana mtaani.
Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku  28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla ya siku  ya kumi na nne na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari, hivyo siku zingine  za hatari  ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.
Kama mzunguko wako ni mrefu labda  siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama mzunguko wako ni mfupi, [ hapa ndio mtu anaeza anabeba mimba kwa kushiriki ngono akiwa kwenye hedhi], mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu. sasa kama mtu huyu anaona hedhi kwa siku nne afu akatembea na mwanaume siku ya nne au ya tatu wakati damu inaendelea kutoka basi mbegu za mwanaume zitaishi mpaka siku ya saba na kukutana na yai la kike ambalo litashuka siku hiyo ya saba na mimba kutunga, hivyo kama hufuatilii mzunguko wako  akibeba mimba siku ya hedhi usishangae.
Mwisho: nimeandika hii makala makusudi kwani najua kuna watu wanatabia za kufanya ngono kipindi cha hedhi au wakati hedhi iko inaisha au tarehe za mwanzo baada ya hedhi kuisha wakidhani mimba haiwezekani basi leo taarifa ni kwamba inawezekana cha msingi fuatilia mzunguko wako vizuri usije ukaanza kusumbua watu ukishanasa mimba ambayo hukuipanga.