Friday, April 27, 2018

HIZI NDIO SABABU TANO KUU ZA KUONGEZEKA WIMBI LA MASHOGA DUNIANI.

niliwahi kuongelea katika moja ya makala zangu kwamba idadi ya wanaume wanaojihusisha na mambo ya ushoga yaani wanaume kuingiliwa kinyume na wanaume wengine linazidi kuongezeka lakini kwenye makala ile nilizungumzia sana kuhusu madhara ya kuingiliwa kinyume na maumbile.unaweza kua unajiuliza sana kwanini wimbi hili linazidi kua kubwa wakati hapo zamani halikuwepo sana.kuna mambo muhimu sana yanayochangia swala hili japokua wengine wanayaapuuzia lakini ni vizuri kuyajua kabla mtoto wako, ndugu au rafiki hajatumbukia huko.
kuiga kutoka kwa watu wengine; asilimia zaidi ya 80 ya watu wanaoingia kwenye vitendo vya kishoga huiga au kufundishwa na watu ambao tayari wako huko.vitendo hivi huanza pale wanapokua wameleweshwa sana au hata katika hali ya kawaida.hivyo kua na marafiki ambao wanajihusisha sana na hivi vitu ni wazi kwamba wewe unavutiwa na maisha hayo na siku moja utakua mmoja wao.siku hizi kuna mpaka group za watsaap za watu wa aina hii wanaendelea kupeana moyo kama vile wanachokifanya ni sahihi sana.
malezi mabaya utotoni; kawaida mtoto wa kiume anatakiwa akuzwe kiume. afanye kazi zote hasa za kiume, avae mavazi ya kiume na muda mwingi akae na wavulana wenzake. kumlea mtoto wa kiume kwa kumpaka make up, kumvalisha nguo za kike na kumchanganya na wasichana katika umri mdogo, kisaikolojia kutamfanya ahisi anaweza kua kama wao na muda sio mrefu utamkosa huyo dume.hii inatokea sana kwa watoto wanaokua bila baba nyumbani.
madhara ya utandawazi; sasa hivi ukiangalia filamu nyingi kutoka marekani zinajaribu kuonyesha kwamba ushoga ni kitu cha kawaida kwa kuonyesha sehemu nyingi za mahusiano ya kishoga.hii hufanya watu wengi kuanza kuona ni kitu cha kawaida sana lakini pia kumetokea wimbi la kutoa ufadhili au urahisi wa watu wa aina hii kusomeshwa bure au kupata nafasi kirahisi hasa vyuo vya nje hii imechangia watu wengine kuingia huko ili kupata nafasi hizo.
fikra potofu;kumekua na fikra potofu kwamba mashoga wanakua wamezaliwa na homoni nyingi za kike, kitu ambacho sio kweli na hali ya mtu kuishi kama mwanamke katika hali ya utoto haina mahusiano na homoni kabisa bali tatizo la kujiendekeza au mtu kupenda kuishi hivyo.mtu anayeishi kike utotoni wakati ni mwanaume anaweza akapata elimu na ushauri na kubadilika.
kutojikubali mwenyewe; siku hizi kuna watu wengi wanabadilisha jinsia zao kua wa kike kabisa hasa nchi za nje au kuna wanaume wanafanya upasuaji ili wawe wanawake kwa kila kitu. huu kitaalamu tunaweza kuita tatizo la kisaikolojia la kutojikubali binafsi kwamba wewe ni mwanaume au wewe ni mwanamke na huwezi kubadili hilo.
mwisho; sijaweka makala hii kupinga au kuukubali ushoga kwani hio sio kazi yangu lakini naaandika makala hizi kuwatahadharisha wazazi ambao wasingependa watoto wao waangukie huko lakini pia kuwaambia wale ambao wako njiani kwenda huko au ambao wako huku tayari waishi wakijua ukweli kuhusu machaguo yao na siku ya mwisho wasije kumlaumu mtu yeyote kwani madhara ya tabia hii ni makubwa sana