''Inavyoonyesha na jinsi ilivyo wanawake huwa wanasema kitu fulani harafu hujikuta wakifanya kitu kingine, vitendo vyao husaliti maneno yao na ndiyo kero kubwa namba moja wanayoikabiri na kuilalamikia wanaume na iwapo ukiwa na uwelewa juu ya hili jambo, litakusaidia kuwa na urahisi zaidi kwenye mchezo wa utongozaji na kuwaelewa hawa viumbe kwa ujumla."
Sababu kubwa inayoleta na kusababisha hamu ya kuwaelewa na kujua kile kinachoendelea kwenye vichwa vya hawa viumbe wa kike wanawake ni sababu rahisi sana; Yule ambaye ataelewa utendaji kazi wa akili za wanawake atakuwa huru kutokana na madhara yatokanayo na mazungumzo nao kama vile hofu ya kukataliwa, hofu ya kuachwa, kutoelewana nao, kuumizwa hisia, kutegwa na kinyongo.
Baada ya miaka elfu moja ya wanaume kutowaelewa wanawake, kiumeni.com imeweza kukata utepe na kupata ufafanuzi kwanini ni vigumu sana kuwaelewa wanawake, ufafanuzi wake hata hivyo siyo mgumu sana, wanawake wanafanana na wanaume kuliko tulivyokuwa tunadhania ila wanatofauti kuu moja inayoleta kasoro kubwa.
Wanawake ni waathirika wa homoni yao kubwa ya Oestrogen ambayo inawafanya wawe na maamuzi ya kutumia hisia zao kuliko viumbe wowote waelewa na hasa yakiwa yanahusika mambo ya kuugusa moyo, siri ya kuwaelewa wanawake na tabia zao zisizoeleweka ni kitu kimoja kikubwa kinachotengeneza fikra zake - Hisia zao.
Hii inaweza kuonyesha jinsi mama anavyopata mshituko mkubwa akiona mtoto ameumia kuliko baba, kwa mfano mama akimkuta mtoto yupo chini ameumia, kimbilio lake la kwanza ni kuuliza nini kimetokea wakati baba akifika kimbilio lake la kwanza ni kumpeleka mtoto hosipitalini.
Kwanini tofauti?, kwa sababu baba mshituko wake wa kwanza ni kumpeleka mtoto hosipitalini harafu kuuliza maswali mengine baadae lakini mama kutokana na kuendeshwa na hisia zinampelekea kutafuta nini kimetokea kwanza au nani kamuumiza mwanaye.
Wanawake wanaendeshwa na hisia kuliko akili, ndo maana wanaume hawatakiwi kuwasikiliza wanawake hasa yakiwa yanahusika mambo ambayo yanagusa hisia zao na moyo wao, hivyo hisia za wanawake hufunika akili yake na bila kujijua anajikuta anafanya maamuzi ya kihisia kwanza na kuacha maamuzi ambayo yanaumuhimu zaidi, ndo maana ukimuuliza mwanamke anapenda mwanaume wa aina gani, atakwambia anapenda mwanaume mpole, mwelewa, aliyeelimika na anayejua kupenda, ila ukimpa muda na kuja kuangalia mwanaume ambae atakuwa naye ni tofauti na maelelezo aliyoyatoa awali, kwahiyo kiuhalisia wanawake hufanya tofauti kabisa na mambo waliokuwa wakisema sababu wanaendeshwa na hisia ambazo humletea fikra tofauti.
Ili uweze kuwa na mafanikio kwenye utongozaji lazima uwe umeshayaelewa haya na kuweka akilini matendo ya wanawake ambayo hayaendani kabisa na maongezi yake na siku nyingine ukiwa umechanganyikiwa na kile mwanamke anachokuambia, fikiria vitu vifuatavyo;
- Wanawake wanafanana na wanaume kuliko unavyofikiri.
- Jiweke katika utata alionao.
- Jiulize ningefanya nini iwapo ungekuwa ni yeye na matarajio ni kwamba atafanya hicho hicho ambacho alichosema hafanyi.
- Usije ukapumbazwa kwa maelezo yake ya kutumia hisia.
- Matendo ndo yakuangalia zaidi kuliko maneno.