"Kupunguza tumbo huitaji mazoezi ya kutosha na siyo kitu cha kuja usiku mmoja, bali ni kwa mazoezi endelevu na ukiweza kumudu kufanya haya mazoezi utaona matokeo yake".
Hamna mtu anayependa kuwa na tumbo kubwa hasa tumbo la kitambi, kila mtu anapenda kuwa na tumbo dogo ambalo huongeza mvuto na kukufanya hata ukivaanguo ikupendeze na kukukaa kwa utanashati zaidi, kiumeni.com wamekukusanyia mazoezi ambayo yatapunguza tumbo lako na yatakuletea maajabu na kulibadilisha tumbo lako kuwa tofauti na kukufanya kila nguo iwe tamu hasa ikiwa imevaliwa na wewe.
RATIBA YA MAZOEZI>>
- Fanya mazoezi haya mara mbili kwa wiki.
- Chukua mapumziko ya sekune 30 mpaka 60 kwa kila seti ya mzunguko wa mazoezi.
- Chukua pumziko la sekunde 60 kwa kila zoezi.
1; Suspended Reverse Crush
Kwa hili zoezi, funga kamba mwisho mwa miguu yako yote miwili, huku ukiwa kwenye mkao wa pushapu, kunja miguu na rudisha kwa urefu kama picha inavyoonesha.
>Fanya seti tano.
>Seti ya kwanza mara 15,
>Seti ya pili mara 12,
>Seti ya tatu mara 10,
>Seti ya nne mara 10,
>Seti ya tano mara 10.
2; Decline Russian Twist
Kaa wima kwenye kiti kilicho binuka kwenye engo ya nyuzi 45, jizungushe upande wa kuria na wa kushoto huku umebeba chuma chenye uzito mdogo kama picha inavyoonyesha.
>Fanya seti 5.
>Rudia mara 12 kwa kila seti.
3; Hanging Leg Raises
Bembea kwenye chuma na nyanyua miguu kufikia urefu sambamba na wa kiuno chako, huku mwili wote ukibaki wima kama picha ndani ya kiumeni.com inavyoonyesha.
>Fanya seti 5,
>Rudia mara 12 kwa seti zote.
Hakikisha unazingatia ratiba ya mazoezi.
- Fanya mazoezi haya mara mbili kwa wiki.
- Chukua mapumziko ya sekunde 30 mpaka 60 kwa kila seti ya mzunguko wa mazoezi.
- Chukua pumziko la sekunde 60 kwa kila zoezi.