Friday, December 22, 2017

Mwanamke Umekuwa na Tatizo la Kutoshika Mimba ? Sababu na Tiba Yake Ipo Hapa

Utafiti wa Chama Cha Madaktari Bingwa wa Akina Mama (FIGO) mwaka 1990 ulionesha kuwa sababu kuu  ya mwanamke kutoshika mimba ni hitilafu katika mirija ambayo kitaalam huitwa Tubal Factor ambapo asilimia 25-35 hutokana na magonjwa ya mirija ya uzazi.
Katika utafiti huo, iligundulika kuwa asilimia 30-40 husababishwa na hitilafu ya kupevuka mayai kitaalam huitwa Ovulatory Factor. Sababu nyingine zilielezwa kuwa ni hitilafu za ukuta wa uzazi, yaani Endometriosis au mwanamke kuwa na uvimbe kwenye mji wa uzazi.
Ile sababu ya matatizo yanayosababishwa na kupevuka kwa mayai au kutotolewa kwa mayai au kutoka kidogo sana, hutokea baada ya vichocheo vinavyoitwa Hormone ya Godotrophins Relising Hormone kutoka sehemu ya tezi la kwenye ubongo ujulikanayo kama Hythalamus kunakosababishwa na tezi kutofanya kazi vizuri.
Kwa sababu hiyo, mayai hutolewa kidogo au kutotoka kabisa na kusababisha baadhi ya wanawake kutoenda kwenye siku zao za hedhi wakati muda wa kufanya hivyo haujafika.
Sababu nyingine zinazofanya mwanamke kushindwa kushika mimba huwa ni kuziba au kuwa na upenyo mdogo wa kusafirisha mayai kutoka kwenye tezi la mfuko wa uzazi, lijulikanalo kitaalam kwa jina la Ovary.
Hali hiyo ya kuwa na upenyo mdogo husababishwa na maambukizi ya bakteria kwenye mirija pamoja na mji wa mimba na tatizo hilo kitaalam huitwa Pelvic Infections. Mwanamke akiwa na tatizo hili atajisikia maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Wanawake wengine hushindwa kupata mimba kutokana na kuwa na hitilafu kwenye mji wa mimba, kama vile kuwa na uvimbe kwenye kizazi au vinyama kuota kwenye mji huo wa uzazi Endometritis au kuwa na matatizo ya kuzaliwa nayo ya mji wa uzazi kuwa mdogo sana.
Tatizo lingine ni mwanamke kuwa na hitilafu kwenye shingo au mlango wa uzazi kitaalam huitwa Cervical Factors,  kama vile maumbile yasiyo ya kawaida, jambo ambalo husababisha usumbufu mji wa kizazi kuwa mbali na uke, hivyo kusababisha ucheleweshaji wa kusafirisha mbegu za kiume Sperms.
Tatizo lingine ni kuwa,  kwenye mlango wa uzazi, huzalishwa utelezi mwingi ambao unaweza kuleta hitilafu katika kufanya kazi.
Sababu nyingine ni mwanamke kuwa na matatizo kwenye uke kama vile kuzaliwa na maumbile ambayo siyo ya kawaida kama kuwa na uke usioshikana yaani Vaginal Septum pia kutokwa na uchafu mwingi Virginal Discharge.
Ili kujua tiba na ushauri wa kitaalam fuatilia wiki ijayo siku kama ya leo.
Mafindo findo
Leo kwenye ukurasa huu tutaangalia tiba ya ugonjwa wa mafindo findo (Tonsils) watu wengi huangaika na gonjwa hili ambalo huambukizwa kwa bacteria hasa kipindi cha baridi, hutokea wakati mwingine kama mafua, kwani huathiri koo, husababisha anayeumwa kushindwa kumeza chakula na hata mate, pia upumuaji wa mgonjwa anapolala huwa ni wa tabu.
Maji ya chumvi
Kama unasumbuliwa na tatizo hili uwe mkubwa au mdogo, tumia maji haya kwa kuchanganya kijiko kimoja cha chumvi na maji ya vuguvugu, kisha sukutua, rudia kusukutua mara kwa mara kwa ajili ya kupata nafuu.
Jinsi ya kutumia Limao kama tiba
Chukua glasi ya maji salama ya kunywa, weka pinch ya Chumvi changanya na juisi ya limao moja, kisha weka kijiko kimoja cha asali, baada ya kupata mchanganyiko huo kunywa kidogo kidogo mara mbili kwa siku.
Bizari
Bizari ya manjano ina uwezo mkubwa wa kumaliza tatizo.
Utumiaji wake
Chukua kijiko kimoja cha unga wa bizari weka kwenye glasi ya maji moto changanya na chumvi kidogo. Ukishapata mchanganyiko huo sukutua mara kwa mara hasa kipindi cha kwenda kulala, itakusaidia kuondoa maumivu.
Mdarasini
Mdarasini unasaidia kutibu tonsils kama utafuatilia kutumia kitiba ni mzuri sana
Jinsi ya kutumia
Chukua kijiko kidogo cha unga wa mdarasini, weka kwenye maji ya moto.
Changanya na vijiko viwili vya asali.
Kunywa taratibu, tumia mara tatu kwa wiki moja.