Friday, December 22, 2017

Mbinu 5 za Jinsi ya Kutongoza Msichana Yoyote Mrembo na Akubali.

Je , unamtamani msichana mrembo ambae kwa sasa ni kama marafiki ? au unavutiwa na yule demu unayemuona kila siku mtaani na unashidwa kujizuia sema hujui uanzaje ? Haijalishi kama unamjua au hamjuani , ila inapokuja kwenye kumtongoza mwanamke unachotakiwa kujua ni uelewa wa vitu kadhaa kuhusu jinsi kutamani kunavyokua na jinsi ya kufanyia kazi ili ufanikiwe .

Kumtongoza demu na vitu unavyotakiwa kujua

kwanza kabisa kama unataka kumtongoza msichana au kumfanya tu akupende tu , inabidi uwe mtu poa ambae anaweza kuvuta macho ya wasichana.

Kama hautaweza kua mtu anayeweza kumvutia msichana kirahisi , utakua bado unauwezo wa kumtongoza mwanamke unayempenda lakini itakua ngumu kuwezesha yeye akukubali .

Kiufupi fatisha njia hizi 11 rahisi na kiukweli kabisa utakua vizuri katika kutongoza na hata kwa mambo mengine yatakayofuata baada ya hapo.

Tumia njia hizi moja baada ya nyingine na ijapokua utacheza karata zako vizuri basi lazima umpate mrembo yoyote unayemtaka hata kama kuna watu wengine kibao wanamfukuzia .

1 . Kua karibu nae

Siku zote , kama unataka kumtokea msichana njia muhimu kabisa ni kuweza kumjua kwa undani .Usikurupuke kurupuke tu ukaanza kutongoza , msichana ataogopa au atakuona mtu rahisi kua nae na mwisho wa siku utaishia kumboa tu .

Ongea nae na upate kumjua vizuri . Mtumie message na usiwe na mzuka , mfanye awe kama rafiki kwanza . Usimtokee kwanza sema pia usisubiri sana maana ataanza kukuchukulia poa .

2 . Kua mtu unayependeka

Hii ni hatua muhimu sana . Na huu ndio wakati utagundua kama anahisia na wewe kweli au anakuchezea akili . Pia unapoongea nae mara kwa mara jaribu kugundua vitu anavyovipenda. Jaribu kuweka ukaribu nae kwenye kitu ambacho wote mnakipenda.

3 . Usilale Usiku

Ndio maana mitandao mingi ya simu ikawapa ofa za usiku watu kama nyie muongee usiku kucha . Usiku ndio muda sahihi wa kuweza kutoa ya moyoni na kueleza hisia zako kwa msichana . Anza kwa kuweka maongezi ya kawaida na kadiri unavyoendelea weka vionjo fulani vitakavyomfanya aanze kuingia line bila kugundua kama unamtokea.

4 . Ishi Maisha mawili

Unapoongea nae usiku , mwaga sera zako na funguka kuhusu mambo ya mapenzi sema mkikutana ana kwa ana mchana usiongelee mambo ya mapenzi kabisa labda aanze yeye na hivyo kumaanisha ashaingia line na anapenda maongezi hayo .

Pia epuka kuongelea kuhusu mambo yenu ya kimapenzi mnapokua na marafiki wengine bali fanyeni hivyo mkiwa wawili . Kwa kufanya hivyo unamfanya aamini kuna uhusiano motomoto wa siri unapikika kati yenu.

5 . Usimfanye ajue unampenda

Wanaume wengi ufanyaga kosa hili kubwa . Wanawaambia wanawake wanawapenda au wanahisia za kimapenzi kwao . Ni kweli unampenda , anajua hivyo tayari . Au hajui ? Unampigia simu kila saa , mnataniani kimapenzi na anaona uhusiano wenu kabisa .

Kwahiyo japokua anahisi unampenda , usije kuonyesha hivyo kwani anahitaji kusikia kutoka kwako ili ajihakikishia hisia zake . Chukulia poa na usifunguke kuhusu hisia zako kwake , kitendawili alichonacho ndicho kitamfanya azidi kukunata na kutaka kujua mwisho wa mambo