Sunday, November 19, 2017

WEWE MWANAUME, HUO UGUMU NA KUTOTAKA KUELEKEZWA KITU NA MPENZI WAKO KUNATOKA WAPI??


Tafiti zinaonyesha kwamba wanawake wameumbiwa ndani yao ujuzi wa asili wa namna gani mahusiano yanatakiwa yawe,  namna gani ndoa inatakiwa iwe na pia familia na malezi yaweje, wao hawahitaji sana mafunzo na kama mafunzo yanakuwepo basi nikuongezea kile walichonacho tayari. Wanaume wao huhitaji kusaidiwa kujua namna ya kuishi kwenye mahusiano, ndoa na hata namna ya malezi. Kusaidiwa au kufundishwa huku huanzia toka kwa wazazi wa mwanaume huyu na mara nyingine hata mke wake huwa na maeneo ya kumfundisha na kumsaidia zaidi pia. Iwapo mwanaume hakupata nafasi ya kujifunza, kufundishwa toka kwa wazazi la labda hayuko tayari kufundishwa au kuelekezwa na mke wake basi anaweza kuwa mtu mbovu sana na wenye kuudhi katika mahusiano na mambo ya familia. Wake zetu, msisite kutufundisha, msidhani tunajua kila kitu, msipotufundisha na kutuelekeza kiukweli mtatuchukia. Na sisi wanaume turuhusu kufundishwa, kuelekezwa na kuwa watii katika kujifunza. Wote wawili ni wadau tulio na hisa sawa katika kuhakikisha tunayafurahia mahusiano yetu, hakuna bwana wala mtwana,,,,,,,,,,,,,