Sunday, November 19, 2017

UZITO WA MWILI, KITAMBI NA UNENE VYAWEZA KUWA NA ATHARI KWENYE MAHUSIANO YAKO

Asikudanganye mtu bwana, uzito mkubwa wa mwili, kitambi na unene vimewanyima wengi sana kuyafurahia mahusiano yao. Najua mara nyingine ni ngumu sana kuwa muwazi kwa mpenzi wako kuhusu uzito wake, unene wake au kitambi chake, na unaona utata kumwambia apungue, lakini hiyo haipunguzi ukweli kwamba haufurahii na unajisikia vibaya, na zaidi ni kwamba unatamani sana apungue. Wala hauhitahi kushurutishwa sana kupungua, faida sio tu kwa mpenzi wako bali kwako pia. Na kama yeye ndicho anachokitamani, inakuwia ngumu nini ku “sacrifice” kwa ajili yake? kwanini kuamua kupungua isiwe zawadi kwake? Najua kuna ugumu, na kuna kujitoa kwa dhati lakini uzuri ni kwamba kujitoa huku kunalipa kwako binafsi na kwa mahusiano yako kwa ujumla – Chris Mauki