Sunday, November 19, 2017

JIFUNZENI KUYAMALIZA SIO KUYAFUKIA




Mara nyingi ni rahisi sana katika mahusiano mkajikuta mnashindwa kuyaongea na kuyamaliza yale yanayoleta misuguano na ukakasi katika mapenzi yenu. Yamkini hamyaongei mkayamaliza kwasababu mnaogopa milipuko, yamkini mnaogopa kupelekea mpasuko au uwezekano wa kuachana, yamkini mmoja anamuogopa mwenzake kwa namna anavyokuwa mkali au mbishi. Kwa vyovyote vile, matatizo baina ya wapenzi yasio ongelewa na kumalizwa na kuwafanya wapenzi kurudi kwenye amani na upendo ni hatari sana. Pale yanapofunikwa na wapenzi kudhani kwamba wamepooza moto, hatari yake nikwamba taratibu hupunguza ladha ya penzi, hupunguza mvuto baina ya wapenzi “intimacy”, kidogo kidogo mnaanza kuchokana, kidogo mnaanza kuangaliana kama mtu na jirani yake na sio mtu na mpenziwe, na msipoangalia au kuwa macho kila mmoja anakosa hamu na hamasa na mwenzake, na hivyo kuweka urahisi wa kutengana. Jifunzeni kuwa na ujasiri wa kuyaongea, jifunzeni kuwa na ujasiri wa kuyaweka mezani na kuhakikisha mnafikia ufumbuzi wa yale yanayowatatiza. Furaha ya kwenye penzi huwekewa mazingira, na haioti tu kama uyoga, au kushuka tu kama mvua