Wednesday, November 15, 2017

WANAWAKE : HUWA WANAANGALIA WENYE MAFANIKIO.


Ni kama miongo mitatu sasa wanaharakati wamejitahidi kuwafanya wanaume wajisikie aibu kuvutiwa kimwili na mwanamke anayevutia katika mwonekano wake.
Ingawa ni kweli wanaume walizaliwa kuona (born to see).
Ni kweli huvutiwa na kushtuka pale mwanaume akikutana na mwanamke anayependeza na kuvutia.
Macho mwanaume yanauwezo wa kuona (scanning) mwanamke anayevutia katika kundi la mamia ya Wanawake utadhani macho yana lensi za kivita kwa ajili ya kurusha makombora kwa usahihi.
Au mwanamke anayevutia akipishana na mwanaume (si wote) lazima afanye juhudi ya ziada kuhakikisha mboni ya jicho inakaza kule alikuwa anaangalia vinginevyo anaweza kusababisha ajali.
Tukija suala la Wanawake; ingawa wao hukataa ukiwauliza ila ndani yao ukweli hujieleza kwamba mwanamke huvutiwa na mwanaume kutokana na mafanikio au uwezo alionao katika jamii.
Kuna usemi wa kingereza kwamba:

“Men are evaluated by income and professional status while women are evaluated by their looks”

Hii ina maana mwanamke na mwanaume wapo wired tofauti linapokuja suala la kumpata mwenzi au mtu wa kuishi naye pamoja.

Mwanaume hutafuta mwanamke ambaye anavutia, mwanaume huona uzuri wa mwanamke kuliko akili ya mwanamke kichwani mwake.

Mwanamke hutafuta mwanaume ambaye ana mafanikio, mwanamke huona akili ya mwanaume kuliko uzuri wake wa sura.

Ndiyo maana kuna utani kwamba mwanaume akiwa na pesa hata kama ana sura inayofanana na chimpanzee bado Wanawake watamuona ni handsome wa nguvu.

Je, ukiwachukua mabinti wanaomaliza chuo na kuwauliza kama wapo tayari kuolewa na mwanaume ambaye atakuwa na kipato cha chini kuliko wao watakubali?

Je, ukimuuliza binti yeyote ambaye ana taaluma yake na anataka kuolewa kama atakubali kuoana na mwanaume asiyevutia ila ana kazi nzuri na kipato cha uhakika?
Si rahisi kwa mwanamke kukubali kwamba anahitaji mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha ili aoane naye ingawa katika ukweli mwanaume mwenye mafanikio au akili ya maisha humfanya mwanamke kujiona yupo protected, ni mwanaume ambaye anayeonekana anaweza kuwajibika au kwa lugha nyingine si pesa alizonazo bali ule uwezo wa kupata pesa alionao ndiyo humvutia mwanamke.

Ndiyo, wapo wanawake huvutiwa na wanaume walichacha (pigika) au wengine hubeba mwanaume yeyote hata hivyo mwanaume kuwa na pesa ni sexy na mwanamke anajua kuwa na mwanaume asiye na akili ya maisha au uwezo kifedha atatumia muda wake kuishi naye huku akiwa na hofu na mashaka kuhusu pesa.
Kwa wanawake wengi “money is security” najua utabisha ila ndo ukweli!